TAVA YAZINDUA VITUO VYA MAFUNZO YA WAVU NCHINI TANZANIA
CHAMA cha wavu Tanzania (TAVA) kushirikiana nachama cha wavu Afrika(CAVB)
pamoja na shirikisho la wavu Duniani( FIVB) wamefanikiwa kuzindua vituo vya
kufunziavijana (wasichana) mchezo wa wavu nchini .
Mwenyekitiwa kuendeleza mchezo wa wavu mashuleni na vyuoni Amoni Safieli
alieleza kuwa mpaka sasa tayariwamefanikiwa kufungua vituo vitatu nchini
ambavyo ni pamoja na kituo kilichopo shule ya sekondari Tanga,Masasi
sekondari –Mtwara nakituo cha shule ya msingi Manyara Ranch(Manyara Ranch
primary school centre)kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha .
“Tunatarajiakuwa na vituo vine vya kufunzia vijana hususani watoto wa kike
wa mchezo huu nchini ambapo mpaka sasa Tayaritumefanikisha kufungua vituo
vitatu nakituo cha nne tutakifunmgua mkoani Dodoma mda wowote ili kuweza
kukamilishazpezi hili tayari kabisa kwa mafunzo kwa vijana .”alieleza
Safieli.
Safieli alielezakuwa lengo kuu ni kuhakikisha vipaji vya watoto vinaanzishwa
wakiwa mashuleniili kuweza kuwa na wachezaji ambao watakuwa tayari
wamelelewa na waalimu nawataalamu waliobobea katika mchezo huo.
“Kila kituo tulichozinduatuilifanikiwa kutoa vifaa vya mchezo huoambavyo ni
mipira 200 pamoja na vyavu 8 ambapo vilikuwa na thamani ya shilingimilioni
50 kwa kila kituo tulichofika kuzindua mradi huu ambao umelenga zaidi kwa
wanawake ilikuhakikisha wanakuwa wawakilishi vyema katika mashindano
mbalimbali. ”aliongezaSafieli.
Naye Rais wachama cha wavu Tanzania (TAVA) Agustino Agapa alisema mradi huu
ni kwa wasichana unajulikana kama ndoto za Afrika (African DreamsProject )
utaweza kuhusisha vijana walio na umri kuanzia miaka 8-10 na miaka10-14
ambao watatafuta nchi nzima na watapelekwa katika vituo hivyo ambapo vigezo
mbalimbalivitatumika ili kuweza kuwapata ikiwemo umri na wawe urefu wa
kuanzia sm 170 .
“Matarajioyetu nikuwa baada ya miaka 5 ijayo tuwe na wachezaji bora
watakao wezakuwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ili kuweza
kupeperusha bendera yataifa letu vyema .”alisema.
Agapaalieleza kuwa kila kituo kitaanza kufundisha wachezaji 25 ambao
watafundishwana wataalamu pamoja na wakufunzi waliobobea katika mchezo wa
wavu na ifikapomwishoni mwa mwezi wa kumi wataalamu wa chama cha wavu Afrika
na Shirikisho la wavu Duniani watafika nchini kwalengo la kuja kutenmbelea
vituo hivyo ili kuangalia mahitaji na jinsiya kusaidia
Post a Comment