Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipozi na bango la picha
lenye rangi mbalimbali zinazowakilisha malengo ya dunia 17 kwa Maendeleo
Endelevu wakati wa mdahalo kwenye juma la Umoja wa Mataifa ambalo
linamalizika leo katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja
huo. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere jana.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
RAIS
Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ametoa wito wa kufanyika kwa
mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa Umoja wa Mataifa ili kukidhi
mahitaji ya sasa ya dunia.
Mkapa
alisema hayo jana katika mdahalo kwenye juma la Umoja wa Mataifa ambalo
linamalizika leo katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja
huo. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere jana.
Mkapa
ambaye alichukua muda wake mwingi kuelezea na kuangalia maslahi ya
Umoja wa Mataifa kwa dunia na changamoto inazokabiliana nazo, alisema
kwa muda sasa dunia inataka mabadiliko katika uendeshaji wa Umoja huo
lakini wanaonufaika na mfumo wa sasa wamekuwa wagumu kukubali
mabadiliko.
Alisema
kuna mambo sasa yanatokea yanayohatarisha usalama wa mataifa, lakini
hatua zinazopendekezwa zinashindwa kuchukuliwa kutokana na kuendelea
kuwapo kwa tabia ya vita baridi kati ya mataifa makubwa yenye kura ya
veto katika umoja huo.
Alisema
yeye anaungana na watu wengine duniani wanaotaka mabadilio katika Umoja
huo yatakayozingatia jiografia za kisiasa duniani zinazoweza kusaidia
kuinua uwezo wa utekelezaji wa Vyombo vya Umoja wa Mataifa likiwemo
baraza Kuu na Baraza la Usalama.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipozi na Balozi wa
Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan.
Alisema
kwamba yapo baadhi ya mataifa na wakazi wa dunia hii ambao wanataka
kuondolewa kwa kura ya turufu inayomilikiwa na mataifa kadha kutokana na
makubaliano ya vita kuu ya pili ya dunia.
Alisema
anafahamu kwamba Afrika inakubaliana na suala hilo kimsingi ingawa lina
changamoto yake kwamba nini kitatokea kama kura hiyo ya turufu
itaondolewa.
Hata
hivyo, Mkapa alisema kwamba masuala ya usalama wa dunia ni nyeti sana
kubaki katika mikono ya watu wachache na kutaka uwezo huo kupewa dunia
kwa kuiwekeza katika sheria ya kimataifa inayotaka uwajibikaji wa pamoja
katika masuala ya usalama.
Alisema
katika kongamano hilo la vijana kwamba Afrika imepitisha azimio la
pamoja Machi 8,2005 la kutaka mabadiliko makubwa katika vyombo vya
Umoja wa Mataifa na umoja wenyewe.
Mapendekezo
hayo yaliyotambulika kama makubaliano ya Ezulwini yanataka mabadiliko
makubwa katika uendeshaji wa vyombo vyote vikubwa vya Umoja wa Mataifa
ikiwamo baraza la Usalama, baraza Kuu na ECOSOC.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez na Balozi wa Ujerumani
nchini, Mh. Egon Kochanke.
Alisema
anaomba Mungu mabadiliko hayo yaje kwa kuelewana lakini si kwa sababu
iliyoanzisha Umoja huo na vyombo vyake, vita kuu ya pili ya Dunia.
Alisema
hali bora ya baadae ya dunia kimsingi inategemea ushirikiano wa mataifa
huru kama ilivyoelezwa katika nadharaia zenye uhalisia kamili.
Alisema pamoja na kwamba kunachangamoto nyingi Umoja huo umekuwa jukwaa jema la kuangalia mustakabali wa dunia na wakazi wake.
“Umoja
wa Mataifa umefanyakazi njema kabisa katika maeneo ya misaada ya kiutu,
utunzaji wa mazingira na maendeleo ya jamii na uchumi” alisema na
kuongeza kuwa anasikitishwa na watu wanaoitazama UN katika upande wa
siasa pekee na kulalamikia.
Alisema
Umoja wa Mataifa na mashirika yake wamekuwa wakifanyakazi kubwa na
shughuli zao kwa kipindi kikubwa zimekuwa zikienda vyema kwa
kutoingiliwa na siasa za Baraza la Usalama.
Mkapa
alisema akiwa mwafrika ambaye nchi yake ilishawahi kusimamiwa na Umoja
huo na sasa ina miaka 54 ya Uhuru atakosa shukurani kwa jinsi umoja huo
ulivyohangaika kuondoa ukoloni barani Afrika.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamojan
na Naibu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Kwacha Chisiza.
Alisema kwamba UN imekuwa ikifanya vyema kuandaa mataifa hayo kujitawala.
Aidha
alimpongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kwa juhudi
zake na hasa hotuba yake aliyoitoa Malabo, Equatorial Guinea Juni mwaka
jana wakati alipozindua sherehe za miaka 70 za Umoja wa Mataifa.
Alisema
katika miaka 70 Umoja huo umefanikiwa kutokomeza ubaguzi wa Rangi
barani Afrika, kukabiliana na maradhi na kupambana kutengeneza amani na
kuzuia vita.
Alisema
pamoja na mafanikio hayo miradi na mipango ya maendeleo ambayo yameweka
dunia katika mstari mmoja kama malengo ya millennia na sasa malengo ya
maendeleo endelevu yamefanya dunia kuwa na sauti moja katika kukabili
umaskini na kulinda dunia iwe mahali bora pa kuishi.
Alisema
kutokana na malengo ya millennia watu wanaoishi katika umaskni
wamepungua kwa zaidi ya nusu kutoka watu bilioni 1.9 kwa mwaka 1990 hadi
watu milioni 836 kwa mwaka 2015.
Aidha
mdondoko wa wanafunzi umepungua kwa asilimia 43 kutoka watoto milioni
100 kwa mwaka 2000 hadi watoto 57 kufikia mwaka 2015 na kupunguza pengo
la wasiojua kusoma miongoni mwa wanawake na wanaume.
Aidha
alisema changamoto za vifo na uzazi na uharibiofu wa mazingira kwa sasa
ndio zinazotakiwa kushughulikiwa wakati dunia inaadhimisha miaka 70 ya
uwapo wa Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo akipozi na lengo namba 8
kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Awali
akimkaribisha rais mstaafu kuzungumza, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe alisema wakati umefika kwa
vijana kujua muskabali wa dunia na maendeleo yake.
Alisema vijana ambao kwa sasa ndio wengi wanapaswa kushirikishwa katika kubuni na kutekeleza mikakati ya kimaendeleo.
Naye
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez pamoja na kumshukuru
rais Mstaafu kwa kukubali kuzungumza na vijana katika maadhimisho ya
miaka 70 ya Umoja huo amesema hoja alizotoa rais huyo wa zamani ni za
msingi na zinazostahili kuangaliwa.
Alisema
amefurahishwa na jinsi Kiongozi huyo wa zamani alivyouzungumzia Umoja
wa Mataifa kwa kuangalia mwanzo wake na maazimio ya awali ya kwanini
umoja huo ni muhimu hasa katika suala la amani na usalama.
Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina.
Alisema
hoja aliyozungumza Mkapa ya kuwajibika kwa pamoja kwa amani na usalama
wa dunia na hivyo kushughulikia masuala yenye kuleta tishio kama
mabadiliko ya tabia nchi, umaskini na kuondoa baa la njaa, rais huyo
amegusa vionjo muhimu vinavyotakiwa kuangaliwa.
Aidha
alisema mabadiliko aliyokuwa akizungumzia rais Mkapa ya Umoja huo
ambayo yanatakiwa kuzingatia usalama wa dunia yanawezekana kutokana na
jinsi nchi zinavyowajibika.
Aidha alimshukuru kwa kuzungumzia maendeleo kwanza ya millennia na yale endelevu.
Mratibu
huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kufanyakazi na serikali
ya Tanzania kuhakikiksha kwamba malengo yaliyowekwa ya uwapo wake
yanafanikiwa na watanzania wanaendelea kufaidi program zinazoendeshwa
kwa pamoja kwa manufaa ya ustawi wa nchi.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt. Natalia Kanem na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika
hilo, Christine Kwayu wakipozi na mabango yanayowakilisha kati
ya malengo ya dunia 17 kwa Maendeleo Endelevu.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR), Joyce Mends-Cole pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano
wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.
Kutoka
kushoto ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC), Usia Nkhoma Ledama, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga pamoja na
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania
Hoyce Temu wakipozi na bango la picha lenye rangi mbalimbali
zinazowakilisha malengo ya dunia 17 kwa Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (katikati) akipozi na
vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki mdahalo huo ulioendeshwa na
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa katika Ukumbi
wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana.
Vijana wakiendelea kupozi na namba mbalimbali kati Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) na Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) wakimlaki Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa alipowasili
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akisaini kitabu
cha wageni katika chumba maalum kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere jana jijini Dar. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP)
nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe
akiongozana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa
kuingia kwenye ukumbi wa mikutano. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.
Alvaro Rodriguez wakibadilishana mawazo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Rais mstaafu Benjamin Mkapa
kuzungumza na hadhira iliyoshiriki Kongamano la Umoja wa Mataifa
lililofanyika jana jijini Dar.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa akimshukuru Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe kwa
ukaribisho.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akizungumza Kongamano la
Umoja wa Mataifa lililofanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi
wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akimpongeza Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa kwa hotuba nzuri. Kushoto
ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt.
Mahadhi Juma Maalim akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa kwenye kongamano hilo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa washiriki.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akisoma
maneno yaliyoandikwa kwenye tuzo aliyokabidhi Rais Mstaafu Benjamin
William Mkapa. Kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez
akijianda kukabidhi tuzo hiyo.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kushoto) akimkabidhi Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu Benjamin William Mkapa tuzo ya Umoja Mataifa kwa
kutambua mchango wake katika malengo ya millennia (MDGs) na kuwezesha
Mashirika ya Umoja wa Mataifa kutoa huduma kama taasisi moja.
Anayeshuhudia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard Membe wakati wa Kongamano la Umoja wa Mataifa lililofanyika
jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Mtandao
wa vijana wanaopambana uharibufu wa mazingira (Youth Climate Activists
Network), Fadhili Meta akiuliza swali Je Serikali inamikakati gani ya
kupambana na mabadiliko ya tabianchi?
Mwanafunzi
wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Blesira Mukandala akitoa maoni yake kwa
Umoja wa Mataifa ambapo aliuomba Umoja huo kuwatazama Walemavu kwa jicho
la pili kama makundi mengine yanayofaidika na msaada wa mashirika ya
Umoja huo.
Pichani
juu na chini ni Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa
Tanzania viongozi wa serikali, wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
pamoja na wadau wa maendeleo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
mdahalo huo.
Vijana pamoja na wanavyuo kutoka vyuo mbalimbali nchini wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye mdahalo huo.
Mabalozi
mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na wakuu wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wa maendeleo wakifuatilia
yaliyokuwa yakijiri kwenye mdahalo huo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini walioshiriki mdahalo huo.
Ukumbi
ukiwa umefurika wanafunzi, mabalozi, viongozi wa serikali, wanafunzi na
wadau wa maendeleo wakati wa mdahalo kwenye juma la Umoja wa Mataifa
ambalo linamalizika leo katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa
umoja huo. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere jana.
Maafisa
kutoka UNESCO wakifuatilia mijadala mbambali iliyokuwa ikiendelea
ukumbini hapo Kulia ni Nancy Kaizilege na Rehema Sudi (katikati).
Maafisa
habari na mawasiliano wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
Tanzania Jacqueline Namfua na Sawiche Wamunza wakifurahi jambo ukumbini
hapo.
Meza kuu katika picha ya pamoja na mabalozi waalikwa pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya makundi ya vijana walioshiriki kongamano hilo.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje.
Post a Comment