PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAVA YAZINDUA VITUO VYA MAFUNZO YA WAVU NCHINI TANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
      CHAMA cha wavu  Tanzania (TAVA) kushirikiana nachama cha wavu Afrika(CAVB)   pamoja na shirikisho la wavu Duniani( FIVB)  wamefan...

 

 

  CHAMA cha wavu  Tanzania (TAVA) kushirikiana nachama cha wavu Afrika(CAVB)
  pamoja na shirikisho la wavu Duniani( FIVB)  wamefanikiwa kuzindua vituo vya
  kufunziavijana (wasichana) mchezo wa wavu nchini .



  Mwenyekitiwa  kuendeleza mchezo wa wavu  mashuleni na vyuoni  Amoni Safieli
  alieleza kuwa mpaka sasa tayariwamefanikiwa kufungua vituo vitatu nchini
  ambavyo ni pamoja na kituo kilichopo  shule ya  sekondari Tanga,Masasi
  sekondari –Mtwara nakituo cha shule ya msingi Manyara Ranch(Manyara Ranch
primary school centre)kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha .
  “Tunatarajiakuwa na vituo vine vya kufunzia vijana hususani watoto wa kike
  wa mchezo huu nchini ambapo mpaka sasa Tayaritumefanikisha kufungua vituo
  vitatu nakituo cha nne tutakifunmgua mkoani Dodoma mda wowote ili kuweza
kukamilishazpezi hili tayari kabisa kwa mafunzo kwa vijana .”alieleza
  Safieli.



  Safieli alielezakuwa lengo kuu ni kuhakikisha vipaji vya watoto vinaanzishwa
  wakiwa mashuleniili kuweza kuwa na wachezaji ambao watakuwa tayari
  wamelelewa na waalimu nawataalamu waliobobea katika mchezo huo.
“Kila kituo tulichozinduatuilifanikiwa kutoa  vifaa vya mchezo huoambavyo ni
  mipira 200 pamoja na vyavu 8 ambapo vilikuwa na thamani ya shilingimilioni
  50 kwa kila kituo tulichofika kuzindua mradi huu  ambao umelenga zaidi kwa
  wanawake ilikuhakikisha wanakuwa wawakilishi vyema katika mashindano
  mbalimbali. ”aliongezaSafieli.



  Naye Rais wachama cha wavu Tanzania (TAVA) Agustino Agapa alisema  mradi huu
  ni kwa wasichana  unajulikana kama ndoto za Afrika (African DreamsProject )
  utaweza kuhusisha vijana walio na umri kuanzia miaka 8-10 na miaka10-14
  ambao watatafuta nchi nzima na watapelekwa  katika vituo hivyo ambapo vigezo
  mbalimbalivitatumika ili kuweza kuwapata ikiwemo umri  na wawe  urefu wa
  kuanzia sm 170 .



  “Matarajioyetu nikuwa baada ya miaka 5  ijayo  tuwe na wachezaji bora
  watakao wezakuwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ili kuweza
  kupeperusha bendera yataifa letu vyema .”alisema.



  Agapaalieleza kuwa kila kituo kitaanza kufundisha wachezaji 25 ambao
  watafundishwana wataalamu pamoja na wakufunzi waliobobea katika mchezo wa
  wavu na ifikapomwishoni mwa mwezi wa kumi wataalamu wa chama cha wavu Afrika
  na Shirikisho la wavu Duniani watafika nchini kwalengo la kuja kutenmbelea
  vituo hivyo ili kuangalia mahitaji  na jinsiya kusaidia

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top