PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: POLISI WAZIDI KUMWANDAMA ESTER BULAYA YEYE NA Wafuasi 6 wa CHADEMA Watiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MGOMBEA ubunge Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya, amelala mahabusu katika ...


MGOMBEA ubunge Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya, amelala mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma, akidaiwa kutaka kuvamia Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.
Bulaya, alikamatwa juzi jioni mjini Bunda pamoja na wafuasi sita wa chama hicho, kisha kusafirishwa usiku hadi mjini Musoma. 
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya Bulaya na wenzake kuachiliwa kwa dhamana jana, wakili wa chama hicho, Peter Makole, alisema kukamatwa kwa mwanasiasa huyo ni njama zinazoendelea kufanywa na wapinzani wao ili kumdhoofisha.
Alisema Bulaya na wenzake, wamefunguliwa kesi ya kutaka kujaribu kuvamia kituo cha polisi, jambo ambalo halina ukweli.
Makole alisema Bulaya, alifika kituo cha polisi mjini Bunda juzi saa 11 jioni kwa lengo la kumuona Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Kaunya Yohana, aliyekuwa akishikiliwa kituoni hapo ili kujua sababu za kukamatwa wake. 
Alisema Bulaya na wenzake, wanatarajiwa kufikishwa mahakamni leo. 
Kwa upande wake, Bulaya alisema hizo ni njama za kutaka kumdhoofisha katika kampeni yake ya kuwania ubunge, ambazo haziwezi kumkatisha tamaa, na kuwaomba wapigakura wa jimbo hilo kutotishwa na matukio ya aina hiyo. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top