PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: OLJORO JKT MWENDO MDUNDO KATIKA LIGI DARAJA LA KWANZA, PANONE YASHIKWA PABAYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya JKT Oljoro mwishoni mwa wiki ilitembeza kichapo kutoka kwa timu ya Mbao kutoka mwanza kwa ba...
 
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya JKT Oljoro mwishoni mwa wiki ilitembeza kichapo kutoka kwa timu ya Mbao kutoka mwanza kwa bao 2-0 katika mwendelezo wa ligi daraja la Kwanza.

Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa, Oljoro iliwachukua dakika 5 kupata bao la kwanza mara baada ya mchezo kupitia kwa Laurence Milton, bao ambalo lilidumu kwa dakika 45 za mwanzo.

Mara baada ya mapumziko Timu ya Mbao walikuja juu huku wakikosa mabao mengi, kutokana na safu yao ya ushambuliaji kutokuwa makini katika eneo la hatari.

Hata hivyo Mbao wakijua mchezo huo utakwisha hivyo walijikuta wakiongezewa kichapo zikiwa zimesalia dakika 9 mchezo kuisha, bao lililofungwa na Abdala Bunu baada ya kuwatoka walinzi wa Mbao na kufunga bao safi.

Hadi mchezo una malizika Timu ya Mbao walijikuta wakiambulia Kadi sita za njano na huku Lameck Daniel akiambulia kadi Nyekundu baada ya mchezo kuisha,ambapo haikifahamika kosa alilolifanya.

Katibu Mkuu wa Mbao Richard Atanas mara baada kumalizika mchezo aliwatupia lawama waamuzi kwa kuwakandamiza katika mchezo huo.

“nimelazimishwa kufungwa, Oljoro wapo nyumbani lazima wabebwe, wachezaji wangu wametolewa mchezoni tangu kipindi cha kwanza haiwezekani kadi sita za njano na nyekundu moja zinatolewa bila sababu za msingi kwa kweli maamuzi sio mazuru, na sishangai mtu akiwa nyumbani lazima avune na ndivyo walivyofanya wenzetu” alisema Atanas

Oljoro wanafikisa Pointi 7 wakati Mbao wakisalia na Pointi 4, hivyo mchezo unaofuta Oljoro wanaeleke Dodoma kukutana na JKT Kanembwa ya Kigoma, wakati Mbao watakua nyumbani kuikaribisha Panone Fc ya Moshi ambayo katika mchezo wao mwishoni mwa wiki walilazimishwa suruhu na Geita Goldern Star.

Naye kocha msaidizi wa JKT Oljoro aliongeza kuwa watarajio yao ni kuendelea kufanya vizuri na hatimaye kurejea ligi kuu msimu ujao hivyo sapoti kwa wadau inahitajika zaidi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top