NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu ya
Madini FC ya jijini hapa ambayo inajiandaa na ligi Daraja la Pili (SDL) ngazi
ya Taifa inayotarajia kuannza kutimu vumbi mwezi ujao, inaendelea kujinoa
vikali ili kujiweka fiti zaidi.
Timu ya Madini
itaanzia ugenini michezo miwili, ambapo katika mchezo wao wa kwanza katika
ufunguzi wa SDL itakutana na Allince ya Mwanza, kisha kuendelea kubaki huko
huko kanda ya ziwa ili kuumana na timu ya Rwankoma ya Mara.
Mkurugenzi
wa ufundi wa Madini FC Madaraka Bendera,alisema kuwa tayari timu hiyo
imeshacheza michezo miwili ya kujipima nguvu na kufanikiwa kushinda michezo
yote.
“Katika
mchezo wa kwanza tulishinda 2-1 dhidi ya Machava FC ya Kilimanjaro, na mchezo
wa pili ambao tulicheza wiki iliyopita Mjini Moshi dhidi ya High City SC nao
tulishinda 2-0” alisema Bendera.
Bendera
aliongeza kuwa asilimia 95 timu imekamilika wakati asilimia azilizobaki wakimwachia
Kocha kumalizia kabla ya Kuanza kwa SDL.
“Tumefurahi
kuanza ugenini michezo miwili, itatusaidia zaidi kwasababu michezo ya mwisho
tunakuwa nyumbani kipindi ambacho tumeshajua tufanye nini kwa wakati huo”
aliongeza kusema” Bendera.
Madini FC katika SDL imepangwa kundi B ikwa pamoja na
Alliance FC [Mwanza], AFC [Arusha], Bulyanhulu FC [Shinyanga], JKT Rwankome [Mara], na
Pamba ya Mwanza.
Post a Comment