NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu Ya mastaa wa
zamani wa Jkt Oljoro “JKT Oljoro Old Star” imefanikiwa kuonyesha umwamba wake
mbele ya timu 28 zilizochuana nazo katika ligi ya RPC SABAS Cup baada ya kutwaa
ubingwa wa michuano hayo katika fainali iliyokuwatanisha na Moshono FC kwa
ushindi wa bao 1-0.
Fainali hiyo
iliyopigwa mwishoni mwa wiki katika uwanja vya Sheik Amri Abeid jijini hapa, na
kushuhudiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, timu ya
Kimandolu na FFU ndio zilianza kusaka mshindi wa tatu ambao walitoka suluhu na
kuamuliwa kwa mikwaju.
Timu ya FFU
ilifanikiwa kutwaa nafasi hiyo ya tatu baada ya kuwapiga Kimandolu jumla ya
mikwaju 4-1 na kufanikiwa kupatiwa zawadi ya Jezi yenye thamani ya shilingi
laki 200,000 pamoja na mpira.
Baada ya pambano
hilo ndipo miamba wa JKT Oljoro Old Star walipowabamiza Moshono FC bao 1-0
lililoingizwa kimyani na Samsoni Mwalimga Langa dakika ya 75, na kuwa bingwa wa
michuano hayo na kuzawadiwa jezi ya thamani ya 350,000, kombe pamoja na mpira
huku mshindi wa pili Ambao ni Moshono akizawadiwa Jezi ya thamani ya 300,000
pamoja na Mpira.
Akizungumza wakati
wa kukabidhi zawadi hizo Kamanda Sabas alisema kuwa kutokana na hamasa ya hali
ya juu yaliyojitokeza kwenye mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila mwaka
kuweza kuhamasisha wananchi kushirikiana na polisi katika taarifa za matukio ya
kihalifu.
“Kwa mwaka huu
mashindano haya yanalenga kuhamasisha wananchi kupiga kura kwa amani na utulivu
sambamba na kulinda dhana ya ulinzi shirikishi hivyo niwaombe walioshiriki
michuano hii kuwa mabalozi wazuri huko mitaani kwa ulinzi shirikishi pamoja na
kuhamasisha uchaguzi wa amani na haki” Alisema Kamanda Sabas
Kwa upande wake
mratibu na msimamizi wa michuano hiyo Siku Ernest alisema timu shiriki ni 28
kutoka katika kata 25 za jiji la Arusha pamoja na majeshi ya polisi, magereza
na Jkt oljoro ambao wote kwa pamoja walicheza viwanja vinne vya sokon one,
Aicc, sheika amri abeid na Sinoni.
Post a Comment