PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MADINI FC KUFUNGUA PAZIA LA SDL NA ALLIANCE FC.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya Madini FC ya jijini hapa ambayo inajiandaa na ligi Daraja la Pili (SDL) ngazi ya Taifa inayotara...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya Madini FC ya jijini hapa ambayo inajiandaa na ligi Daraja la Pili (SDL) ngazi ya Taifa inayotarajia kuannza kutimu vumbi mwezi ujao, inaendelea kujinoa vikali ili kujiweka fiti zaidi.

Timu ya Madini itaanzia ugenini michezo miwili, ambapo katika mchezo wao wa kwanza katika ufunguzi wa SDL itakutana na Allince ya Mwanza, kisha kuendelea kubaki huko huko kanda ya ziwa ili kuumana na timu ya Rwankoma ya Mara.

Mkurugenzi wa ufundi wa Madini FC Madaraka Bendera,alisema kuwa tayari timu hiyo imeshacheza michezo miwili ya kujipima nguvu na kufanikiwa kushinda michezo yote.

“Katika mchezo wa kwanza tulishinda 2-1 dhidi ya Machava FC ya Kilimanjaro, na mchezo wa pili ambao tulicheza wiki iliyopita Mjini Moshi dhidi ya High City SC nao tulishinda 2-0” alisema Bendera.

Bendera aliongeza kuwa asilimia 95 timu imekamilika wakati asilimia azilizobaki wakimwachia Kocha kumalizia kabla ya Kuanza kwa SDL.

“Tumefurahi kuanza ugenini michezo miwili, itatusaidia zaidi kwasababu michezo ya mwisho tunakuwa nyumbani kipindi ambacho tumeshajua tufanye nini kwa wakati huo” aliongeza kusema” Bendera.

Madini FC katika SDL imepangwa kundi B ikwa pamoja na Alliance FC [Mwanza], AFC [Arusha], Bulyanhulu FC [Shinyanga], JKT Rwankome [Mara], na Pamba ya Mwanza.

Madini FC inaonekana kupanda kwa kasi tangu ilipotangazwa kuwa mabingwa wa mkoa wa Arusha msimu uliopita na hatimaye kufanya vyema katika ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top