PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KAMANDA SABAS AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu Ya mastaa wa zamani wa Jkt Oljoro “JKT Oljoro Old Star” imefanikiwa kuonyesha umwamba wake mbele ya...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu Ya mastaa wa zamani wa Jkt Oljoro “JKT Oljoro Old Star” imefanikiwa kuonyesha umwamba wake mbele ya timu 28 zilizochuana nazo katika ligi ya RPC SABAS Cup baada ya kutwaa ubingwa wa michuano hayo katika fainali iliyokuwatanisha na Moshono FC kwa ushindi wa bao 1-0.

Fainali hiyo iliyopigwa mwishoni mwa wiki katika uwanja vya Sheik Amri Abeid jijini hapa, na kushuhudiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, timu ya Kimandolu na FFU ndio zilianza kusaka mshindi wa tatu ambao walitoka suluhu na kuamuliwa kwa mikwaju.

Timu ya FFU ilifanikiwa kutwaa nafasi hiyo ya tatu baada ya kuwapiga Kimandolu jumla ya mikwaju 4-1 na kufanikiwa kupatiwa zawadi ya Jezi yenye thamani ya shilingi laki 200,000 pamoja na mpira.

Baada ya pambano hilo ndipo miamba wa JKT Oljoro Old Star walipowabamiza Moshono FC bao 1-0 lililoingizwa kimyani na Samsoni Mwalimga Langa dakika ya 75, na kuwa bingwa wa michuano hayo na kuzawadiwa jezi ya thamani ya 350,000, kombe pamoja na mpira huku mshindi wa pili Ambao ni Moshono akizawadiwa Jezi ya thamani ya 300,000 pamoja na Mpira.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Kamanda Sabas alisema kuwa kutokana na hamasa ya hali ya juu yaliyojitokeza kwenye mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila mwaka kuweza kuhamasisha wananchi kushirikiana na polisi katika taarifa za matukio ya kihalifu.

“Kwa mwaka huu mashindano haya yanalenga kuhamasisha wananchi kupiga kura kwa amani na utulivu sambamba na kulinda dhana ya ulinzi shirikishi hivyo niwaombe walioshiriki michuano hii kuwa mabalozi wazuri huko mitaani kwa ulinzi shirikishi pamoja na kuhamasisha uchaguzi wa amani na haki” Alisema Kamanda Sabas

Kwa upande wake mratibu na msimamizi wa michuano hiyo Siku Ernest alisema timu shiriki ni 28 kutoka katika kata 25 za jiji la Arusha pamoja na majeshi ya polisi, magereza na Jkt oljoro ambao wote kwa pamoja walicheza viwanja vinne vya sokon one, Aicc, sheika amri abeid na Sinoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top