Timu
ya Panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri
wa mafuta ,inatarajia kuanza kutupa karata yake ya mchezo wa kwanza wa
ligi daraja la kwanza (FDL),dhidi ya maafande wa JKT Oljoro ya jijini
Arusha.
Mchezo
huo utafanyika septemba 19 mwaka huu, katika uwanja wa Ushirika mjini
moshi mkoani kilimanjaro,ambapo baada ya mchezo huo pia wataikaribisha
timu ya Polisi Tabora semptemba 26.
Katibu
wa timu ya Panone FC Augstino Mwakatumbula alisema kuwa msimu huu
wanaenda kuanza ligi na kufanaya kila mchezo kwao ni fainali na
watahakikisha wanatinga kucheza ligi kuu msimu wa 2016-2017.
“Tulifanya usajili mzuri wa wachezaji 7 ambao wameungana na wachezaji wetu tuliokuwa nao msimu uliopita"
"tunaimani
wataisaidia timu hii na tuna jumla ya wachezaji 27 wanaounda kikosi cha
timu pia hatukuweza kuwasajili wote waliokuwepo hapo mwanzo kutokana na
matatizo mbalimbali yakiwemo wengine kutokuwa na nidhamu,uwezo wao
umeshuka kimchezo.”alisema Mwakatumbula .
Aliwataja
wachezaji saba ambao wamefanikiwa kusajiliwa na matajiri hao kuwa ni
pamoja na Ally Mseja mchezaji huru na Abdallah Shauri ‘Machopa’ wote
kutoka timu ya Lipuli –Iringa, Florence Haule kutoka academy ya
Kitayosce ya mkoani Kilimanjaro, Frank Kijoti aliyetokea AFC Arusha
Rashid Gumbo kutoka Kinondoni Manispaa ambaao wote ni Kiungo.
Wengine
ni Maulid Khalid kutoka Singida United ambaye ni winga,Mansoul
Mansoul kutoka Coastal Union ya Tanga ambaye ni golikipa.
Timu
hiyo ya Panone FC ipo kambini miezi miwili sasa ikijiweka tayari kwa
ajili ya michuano hiyo ya ligi Daraja la kwanza ambapo inatarajiwa
kucheza michezo ya kirafiki mapema wiki hii na timu za African
sports,Magambo JKT na Coastal Union zote za Tanga .
Panone wananolewa na kocha Atuga Manyundo akisaidiwa na msaidizi wake Azizi Nyoni .
Post a Comment