Uongozi
wa timu ya Coastal Union toka jijini Tanga umesema kuwa hauna mpango wa
kuweka makazi yao Mkoani Arusha kama maneno yanavyozagaa jijini hapa.
Akizungumza
na gazeti hili Ofisa habari wa timu ya Coastal Oscar Asenga, alisema
kuwa hakuna ukweli wowote juu ya kuhamia Arusha licha ya timu hiyo kuwa
na mashabiki wengi kila mkoa.
“tunachopenda
kuwaambia mashabiki wetu hasa wa Mkoa wa Arusha, tutatafuta mchezo wa
kirafiki ambao tutacheza mkoani hapo kabla ya LIgi kuu kuanza nah ii
yote ni kwasababu tunawajali mashabiki wetu wa mikoani” alisema Asenga.
Kauli
ya Asenga inakuja kutokana na maneno yanayo zagaa kwa wakazi wa Arusha
kuwa Coastal Union itahamia Arusha na kufanya Dimba la Sheikh Amri Abeid
kuwa uwanja wao kwa michezo ya nyumbani ili kuhakikisha inavuna mapato.
Baadhi
ya vitu vinavyo sababisha wakazi wa Arusha kuamini maneno hayo ni
kutokana na jiji la Tanga kuwa na timu tatu zitakazo shiriki Ligi kuu
Tanzania Bara msimu wa 2015/2016 ambazo ni Coastal Union, Mgambo na
African Sports iliyopanda daraja msimu wa 2014/2015.
Kwasasa
Arusha haina timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara tangu JKT
Oljoro iliposhuka daraja msimu wa 2013/2014 na kwa sasa ikiwa inapambana
kurudi tena ligi kuu baada ya msimu ulipita kushindwa kupanda na
kuziacha Mwadui ya Shinyanga,na Toto Africans ya Mwanza ambazo zote
zilikuwa kundi moja.
Hata
hivyo wakazi wa Arusha wanaiombea mema JKT Oljoro ambayo inazoshiriki
Ligi daraja la kwanza (FDL) msimu huu ifanye vizuri ili iweze kurejesha
heshima ya Arusha, na katika mchezo wake wa kwanza wa FDL taere 19
septemba, itafungua ligi katika uwanja wa Ushirika na timu ya Panone
kutoka mkoani Kilimanjaro.
Asenga
aliongeza kuwa licha ya timu hiyo kuwa na wachezaji saba wapya
waliosajiliwa msimu huu kutoka ndani na nje ya nchi na kuwa na benchi la
ufundi jipya anauhakika wa kikosi chake kuimalika mapema kabla ya ligi
kuu kuchanganya moto.
Post a Comment