Kipa
aliyewahi kuzitumikia timu Kongwe nchini ikiwepo timu Simba Sc Aman
Simba ambaye kwa sasa ni goli kipa tegemeo katika kikosi cha timu ya JKT
Oljoro amesema ndoto yake kwa sasa ni kuhakikisha timu hiyo inashiriki
ligi kuu msimu ujao.
Kipa
huyo alisema kuwa kila wakati anawaza juu ya Oljoro ili kulejesha
heshima yake na kwa wanajeshi hao ambao wanamwamini kwa kuwapa ushauri
wachezaji wenzake hasa wale chipukizi.
“nimekuja
hapa ili kupambana na kuhakikisha kila mtu anaijua Oljoro, hii ni timu
mpya kwangu ila mimi sio mgeni kwenye soka la Bongo na ndio maana kila
wakati nawasihi wenzangu tupambane, kwa sababu hii ndio ofisi yetu hivyo
loazima tuithamini ofisi” alisema Simba.
Kwa
upande wake Kocha msaidizi wa Timu hiyo Joery Mwambelele alisema kuwa
Aman Simba amekuwa msada mkubwa kwa timu hiyo, hasa kwa upande wa
nidhamu na wenzake hujifunza kupitia kwake.
“wachezaji
wazoefu ambao wengi tunawaita wakongwe wanapofika katika timu change
kama hii huwa wanaongoza kuwa na nidhamu mbaya lakini kwa Aman Simba
yeye yupo tofauti kabisa, kwanza sio muongeaji halafu anamuheshimu kila
mtu hapa, najivunia kuwa na mchezaji wa namna hii” alisema
Timu ya Oljoro inafungua pazia la FDL septemba 19 na timu ya Panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri wa mafuta katika uwanja wa Ushirika uliopo Moshi
Ligi daraja la kwanza ina shirikisha jumla ya timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu ambapo timu ya Oljoro ipo
katika kundi ‘C’ na timu za Pnone- moshi,Polisi Mara –Mara,Rhino
Rangers –Tabora,Mbao fc –Mwanza,Polisi Tabora -Tabora,Geita Gold –Geita
na JKT Kanembwa – kigoma .
Post a Comment