PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: AMAN SIMBA: NATAKA KUILEJESHA OLJORO LIGI KUU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA YOHANA CHALLE.  PRINCEMEDIATZ Kipa aliyewahi kuzitumikia timu Kongwe nchini ikiwepo timu Simba Sc Aman Simba ambaye kwa sasa...
 


Kipa aliyewahi kuzitumikia timu Kongwe nchini ikiwepo timu Simba Sc Aman Simba ambaye kwa sasa ni goli kipa tegemeo katika kikosi cha timu ya JKT Oljoro amesema ndoto yake kwa sasa ni kuhakikisha timu hiyo inashiriki ligi kuu msimu ujao.

Kipa huyo alisema kuwa kila wakati anawaza juu ya Oljoro ili kulejesha heshima yake na kwa wanajeshi hao ambao wanamwamini kwa kuwapa ushauri wachezaji wenzake hasa wale chipukizi.   

“nimekuja hapa ili kupambana na kuhakikisha kila mtu anaijua Oljoro, hii ni timu mpya kwangu ila mimi sio mgeni kwenye soka la Bongo na ndio maana kila wakati nawasihi wenzangu tupambane, kwa sababu hii ndio ofisi yetu hivyo loazima tuithamini ofisi” alisema Simba.

Kwa upande wake Kocha msaidizi wa Timu hiyo Joery Mwambelele alisema kuwa Aman Simba amekuwa msada mkubwa kwa timu hiyo, hasa kwa upande wa nidhamu na wenzake hujifunza kupitia kwake.

“wachezaji wazoefu ambao wengi tunawaita wakongwe wanapofika katika timu change kama hii huwa wanaongoza kuwa na nidhamu mbaya lakini kwa Aman Simba yeye yupo tofauti kabisa, kwanza sio muongeaji halafu anamuheshimu kila mtu hapa, najivunia kuwa na mchezaji wa namna hii” alisema

Timu ya Oljoro inafungua pazia la FDL septemba 19 na timu ya Panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri wa mafuta katika uwanja wa Ushirika uliopo Moshi


Ligi daraja la kwanza ina shirikisha jumla ya timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu ambapo timu ya Oljoro ipo katika kundi ‘C’ na timu za Pnone- moshi,Polisi Mara –Mara,Rhino Rangers –Tabora,Mbao fc –Mwanza,Polisi Tabora  -Tabora,Geita Gold –Geita na JKT  Kanembwa – kigoma .


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top