PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: AJTC WATWAA UBINGWA SHINDANO LA VYOMBO VYA HABARI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ KIKOSI imara cha chuo cha uandishi wa habari Arusha AJTC kilichotwaa ubingwa wa michuano ya vyombo ...

NA YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ
KIKOSI imara cha chuo cha uandishi wa habari Arusha AJTC kilichotwaa ubingwa wa michuano ya vyombo vya habari lililofanyika  hivi karibuni   katika viwanja vya sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha. Picha NA HABABI MOHAMMED


Chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha (AJTC) mwishoni mwa wiki kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za michezo mkoani Arusha (TASWA)

Mashindano hayo yaliandaliwa kwa lengo ikiwa kuhamasisha uchaguzi wa amani,huru na wa haki hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Urais,Wabunge na madiwani.

Mashindano hayo yalichezwa kwa mfumo wa ligi na AJTC walitwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 7 wakifuatiwa na ORS Radio ya Manyara ilikuwa na pointi 4.

Pamoja na AJTC na ORS Radio timu nyingine zilizoshiriki ni TASWA Dar es salaam, TASWA Arusha, MJ radio, na Arusha One FM.

Mwenyekiti wa TASWA ,Musa Juma alizipongeza timu zote kwa ushiriki wao hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa letu lina elekea katika uchaguzi mkuu mwezi wa kumi mwaka huu.

“napendsa kuwasihi waandishi wenzangu na wananchi wote kuhakikisha wanapiga kura na kumchagua kiongozi atakaye leta maendeleo na kuwajari watanzani bila kubagua” alisema Juma.

Aliongeza kuwa waandishi wanahitajika kutumia vizuri kalamu zao katka kuwaelimisha wananchi juu yauchaguzi hna sio kuwapamba wagombea kwenye vyombo vya habari.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top