mchezaji
wa timu ya wavu ya Mkoa wa Tanga wanawake waliovaa jezi ya Bluu akipiga mpira
katika mashindano ya wavu klabu bingwa Tanzania katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid Arusha kati ya Dodoma wanawake na Tanga yaliyomalizika mwishoni mwa wiki,
Tanga walishinda kwa seti 3-0. Picha na Yohana Challe
TIMU zaa JKT
Mbweni kutoka Dar es salaam kwa wanaume na wanawake zimefanikiwa
kuchukua ubingwa wa wavu Tanzania msimu wa 2015 baada ya kufanya vyema katika
mashindano ya klabu bingwa wavu yalilomalizika mwishoni mwa wiki jijini
hapa.
Mashindano hayo
yaliyoendeshwa kwa mtindo wa ligi yalimalizika kwa timu kwa wanaume timu ya Jkt
Mbweni kunyakua ikiwa na jumla ya pointi 15,ikifuatiwa na timu ya Tanga
ilijikusanyia jumla ya pointi 12,nafsi ya tatu iliwaendea timu ya Pentagone ya
Arusha kwa pointi 9 ,huku Dodoma wakipata jumla ya pointi 6 ,Karatu pointi 3 na
timu ya Flowers Arusha ikikosa pointi na kushika mkia.
Maafande hao wa
JKT Mbweni pia kwa wanawake walimaliza mashindano hayo wakiwa na pointi 6 wakifuatiwa
na Tanga kwa pointi 3 huku Dodoma nao wakimaliza bila pointi.
Michuano hiyo ya
Klabu Bingwa wavu Tanzania ilichezwa kwa siku tatu katika viwanja vya
sheikh amri abeid pamoja na viwanja vya pentagon klabu, huku ikiwa chini ya
chama cha wavu mkoa wa Arusha (AVA) Pamoja na chama cha wavu Tanzania (TAVA).
Akifunga
mashindano hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoaa wa Arusha, Mwanvita O. Okeng’o
ambaye ni afisa michezo mkoa aliwasihi wacheze mbalimbali kuongeza juhudi
katika kuhakikisha wanahamasiha mchezo wa wavu unakuwa na wachezaji wenye uwezo
wa hali ya juu.
Naye Makamo
mwenyekiti wa chama cha wavu Tanzania (TAVA) Muharini Mchume alieleza
kuwa pamoja na kuwa timu sita pekee ndizo zimechuana vikali zimeweza kuonyesha
ushindani wa kipekee kwani zilionekana kuchuana vilivyo.
“Mashindano
yamekwenda vizuri natunawashukuru chama cha wavu Arusha (AVA) kwa
maandalizi makubwa yaliyowezesha kufanyika kwa michuano hii vile vile shukrani
kwa wazamini mbalimbali waliojitokeza kutuunga mkono” alisema Mchume
Aliongeza kuwa
mwenyekiti wa chama cha wavu Tanzania (TAVA) Augostino Hagapa hakuweza
kufika kutokana na kuteuliwa kuwa ‘Match Commissioner” katika mashindano ya
wavu ya All Africa Games yanayotarajiwa kuanza mapema mwezi septemba
nchini Congo,akimuwakilisha Rais wa shirikisho la wavu Afrika.
Aidha chama cha wavu
mkoa wa Arusha kimekabidhiwa mipira mitatu na chama cha wavu Tanzania (TAVA) vile
vile kilimkabidhi mgeni rasmi mpira mmoja kwa ajili ya mazoezi.
Mabingwa watetezi
wa michuano hiyo ya wavu 2014 timu ya Magereza kwa wanawake kutoka jijini
Dar es salaam pamoja na timu ya BOT ya jijini Mwanza kwa wanaume nazo pia
hazikuweza kufika na kutetea ubingwa wao.
Post a Comment