Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula akimkabidhi
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi nakala ya kitambu kinachoelezea kwa kina historia ya Chuo Kikuu
cha Dodoma. Katika Maelezo yake, Prof. Kikula amesema UDOM imeamua
kuweka katika maandishi historia nzima ya Chuo hili ili kuepusha
upotoshaji na upindishaji wa ukweli na kwamba UDOM inapanga kumuenzi
Mhe. Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni kutambua mchango wake katika
kuanzishwa na hatimaye ujenzi wa UDOM. wengine katika picha kutoka
kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Prof. Shaaban Mlacha anayesimamia masuala
ya mipango, fedha na utawala, Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi
Ramadhan Mwinyi na Bi. Christina Silvester, Katibu wa Baraza.
Makamu
Mkuu wa UDOM Prof. Kikula akimkabidhi nakala ya kitambu cha historia ya
UDOM, Prof. Estomih Mtui, M.D anayefanya kazi Weill Cornel Medical
Collage, Prof. Mtui ni moja kati ya wana-Diaspora ambaye amekuwa
kiungo kikubwa katika utafutaji na upatikanaji wa vifaa tiba ,vitabu na
wataalam wa fani mbalimbali kwaajili ya kusaidia nchini Tanzania.
baadhi ya vifaa na vitabu ambavyo Ujumbe wa Makamu Mkuu wa UDOM
wamevikagua vimepatikana kwa juhudi za Prof. Mtui
Na Mwandishi Maalum, New York
Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM), kinatarajia kufanya hafla ya aina yake ya kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya kutambua mchango wake wa hali na mali uliopelekea kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho cha aina yake
Tanzania na nje ya Tanzania.
Taarifa ya kusudio la Chuo hicho kumuenzi Mh. Rais Kikwete imetolewa mwishoni mwa wiki na Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Idris Kikula wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi na Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa.Profesa Kikula na ujumbe wake yuko katika ziara ya kikazi nchini Marekani, ziara iliyomfikisha Jijini New York, ambapo ujumbe ulipata fursa ya kukagua vifaa tiba na vitabu vya kiada na ziada ambavyo vimetolewa na wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na Tanzania.
Baada ya kukagua vifaa na vitabu hivyo na kijiridhisha, Makamu Mkuu wa UDOM ameushukuru Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwa kuwapatia fursa hiyo ya kujionea wenyewe aina ya vifaa tiba na vitabu ambayo amesema vitakuwa msaada mkubwa kwa Kitivo
cha Sayansi ya Afya cha Chuo hicho.“Waheshimiwa Mabalozi, mimi na ujumbe wangu napenda kwa moyo wa dhati kabisa kutoa shukrani zetu kwa kutuonyesha vifaa na vitabu ambavyo kupitia kwenu wafadhili wamevitoa kuwasaidia watanzania nanyi mkaona bora kutushirikisha na kuona namba gani Chuo chetu kinaweza kunufaika na misaada ya aina hii” akasema Pofesa Kikula
Na kuongeza kwamba Kitivo cha Sayansi ya Afya na ambacho pia kina Zahanati kinahitaji sana misaada ya kila aina ili kiweze kutimiza lengo lake kuu la kuwaandaa madaktari na wataalam mbalimbali lakini pia kutoa huduma uchunguzi na matibabu siyo tu kwa wanafunzi na wafanyakazi wa UDOM bali pia kwa watanzania wote.
“ Uongozi wangu unapenda kutambua juhudi zenu hizi za kushirikiana na wadau mbalimbali kusaidia siyo tu vyuo vikuu vyetu lakini na watanzania.Mmedhihirisha kwa kwa vitendo na si
maneno na hii imetupa faraja sana na kudhihirisha namna gani tunaweza kushirikiana kwa karibu Zaidi.
Akasema kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma ni ndoto na hatimaye mbegu iliyopandwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete , ndoto uliyoanzia kwenye kampeni yake ya urais mwaka 2005.
“ilianza kama ahadi ya kampeni, ahadi ambayo haikuishia katika maneno matupu ya ahadi bali aliitekeleza ahadi ile na leo hii tunaiona mbegu aliyoipanda ikichanua na mavuno yanaonekana”. Akasema Prof.Kikula kwa msisitizo wa aina yake.
Anasema haikuwa rahisi kuifanikisiha ndoto ile ya Rais kutokana na pingamizi mbalimbali kutoka nje na ndani ya serikali.
Anaongeza kuwa shauku ya ujenzi na hatimaye uwepo wa UDOM haukuishi kwa watanzania tu bali hata baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania ambazo walikuwa wa kimfuata na kutaka kujua tajiri ngani aliyekuwa anafadhiri mradi huu mkubwa.
Profesa anasema mara zote alikuwa akiwajibu Mabalozi hao kuwa mradi ule ulikuwa ukijengwa na kufadhiliwa na watanzania wenyewe na serikali yao.
“Nisema kwamba haikuwa kazi rahisi, tulipata wakati mgumu na pingamizi hata kutoka ndani ya serikali. Wapo baadhi ya viongozi ambao hawakutaka Chuo Kikuu hiki kijengwe Dodoma.
Mimi binafsi nilimuuliza Mhe. Rais kwa nini alikuwa anataka Chuo Kijengwe Dodoma.Mhe. Rais alinijibu. “Ninataka kijengwe Dodoma na si kwingine, kwa sababu kwanza, ya
umaskini wa Mkoa wa Dodoma na pili Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi”.
Profesa Kikula anaeleza kuwa Mhe. Kikwete aliamini kwamba kwa kujenga chuo Kikuu chenye ukubwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wengi Zaidi, pamoja na kuongezaudahili wa
wanafunzi wengi na kuwapa fursa vijana wengi wa kitanzania kupata elimu ya juu, lakini pia kungefungua milango ya kiuchumi na maendeleo ya kijamii, na hivyo kuwapunguzia umaskini
wananchi wa Mkoa wa Dodoma.Kwa mijibu wa Makamu Mkuu wa UDOM anasema, maono hayo ya Rais ya kuongeza udahili wa
wanafunzi na kufungua milango ya uchumi na kupunguza umaskini kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Ni kwa sababu hiyo, Profesa Kikula anasema, watanzania hawanabudi kujivunia mafanikio yanayotokana na utekelezaji wa ahadi na vipambaumbele vinavyowekwana serikali yao.
“watanzania ni vema tukajijengea utamaduni wa kujivunia mafanikio yetu, penye ukweli lazima tusema, sisi wa Chuo Kikuu cha Dodoma tuna kila sababu ya kujivunia mafanikio ya Chuo hiki, na ndio maana tumeandika kijitabu kinachoelezea historia ya UDOM na mchango mkubwa
wa Mhe. Rais. tumeweka kwa maandishi ili kuepusha upindishwaji ukweli na upotoshaji wa
historia ya UDOM”.Akasema kuwa tayari kijitabu hicho amekabidhiwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kwaajili ya hatua za kuangalia taratibu za kumuenzi Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa upande wake, Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wakudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ameushuku uongoziwa UDOM kwa kuitikia wito wa Uwakilishi wa kutumia ziara
yao ya kikazi, kujionea kukagua vifaa na vitabu ambavyo vimepatika kwa ushirikiano wa Uwakilishi na wadau mbalimbali.
Akasema kuwa Uwakilishi utaendelea na juhudi za kutafuta wadau wanaoweza kusaidia katika maeneo mbalimbali, kutokana kwamba wapo watu wanaopenda sana kuisaidia Tanzania,
akasisitiza haja na umuhimu waufuatiliaji na wepesi wa kujibu barua au mapendekezo
Uwakilishi unapeleka kwa Taasisi mbalimbali zikiwa Vyuo vya elimu ya Juu.
Post a Comment