Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Raisi Jakaya
Kikwete amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha kuwa wanajenga
barabara maeneo ya vijijini ili kuchochea maendeleo katika maeneo ya vijijini na kufungua fursa
mbalimbali za kiuchumi zilizoko katika maeneo hayo.
Kikwete
amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa Viongozi wa serikali za mitaa
(TAMISEMI) uliowakutanisha wakuu wa mikoa,wilaya,Pamoja na Wakurugenzi kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa ubora wa
kazi na barabara endelevu,Raisi Kikwete
amesema kuwa ujenzi wa barabara vijijini utafungua milango ya maendeleo
vijijini na kubadilisha maisha ya watu wengi
Pia Rais
Kikwete amewataka Viongozi wa Serikali za mitaa kuwa waaminifu katika kusimamia
mfuko wa barabara ambao umefikia kiasi cha shilingi bilioni 800 ili mfuko huo
uweze kuwahudumia Watanzania badala ya kuwanufaisha watu wachache.
“Fedha hizi
za mfuko wa barabara zikitumika vizuri zitapunguza matatizo ya miundombinu ya
barabara yanayozibili sehemu nyingi nchini” Alisema Kikwete
Waziri wa
TAMISEMI ,Hawa Ghasia amesema kuwa wizara yake imeanzisha idara kamili ya
Miundombinu ambayo itafanya ukaguzi na kuzuia hasara inayotokana na ujenzi wa
barabara chini ya kiwango.
Ghasia
alisema kuwa kumekua na changamoto ya fedha inayokwamisha ukarabati wa barabara
za mitaa ambazo husiadia upanuzi wa miundombinu katika maeneo mbali mbali.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya TAMISEMI ,Jumanne Safini amesema
kuwa Wizara hiyo inakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa rasilimali za kutosha hali inayosababisha viwango duni vya barabara
vinavyotokana na kukosekana kwa usimamizi na ukaguzi hivyo kutopata barabara endelevu.
Post a Comment