Ndugu Jumaa Aweso.
Na Mohammed Hammie, Pangani, Tanga
Mtoto
wa mama ntilie mwenye uzao halisi kutoka wilayani Pangani mkoani Tanga,
Ndugu Jumaa Aweso (pichani) ameibuka na ushindi wa kishindo katika
uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi CCM.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo katibu wa CCM wilayani Pangani Bi Zaina Mlawa
amesema kuwa, katika uchaguzi huo uliowashirikisha wagombea wapatao kumi
na moja, Ndugu Aweso amekuwa wa kwanza miongoni mwa wagombea hao.
Uchaguzi
huo uliokuwa na ushindani wa aina yake kutokana na kuwepo kwa aliyekuwa
Mbunge wa jimbo hilo Ndugu Salehe Pamba, uliwashirikisha wapiga kura
wapatao 10376 wa chama cha mapunduzi.
Awali
wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Bi Zania aliwataja wagombea
hao kwa idadi ya kura walizopata na kusema kuwa "Ndugu Wahi Ibrahim
amepata kura 87, ndugu Rosemary Luanda amepata kura 89, ndugu Elizabeth
Alatanga amepataa kura 158, Halima Kimbau amepata kura 222, Ndugu
Mohammed Rished amepata kura 442, Ndugu Ayubu Mswahili amepata kura 565"
Bi
Zania ameongeza kwa kusema kuwa "Ndugu Omary Mwidadi amepata kura 587,
ndugu Omary Chambega amepata kura 720, ndugu Salehe Pamba amepata kura
1567, ndugu Abdurahmani magati amepata 1956, na ndugu Jumaa Aweso 3983"
Ushindi
huo kwa ndugu Jumaa Aweso unampa nafasi ya kuwa mgombea wa kwanza
katika kuipeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Pangani
endapo kamati kuu ya maamuzi itaridhia.
Mpaka
sasa katika jimbo la Pangani kumepatikana wagombea wawili ambao
wanaonekana kupendwa sana na wanancho ambao ni Amina Mwidau wa CUF
pamoja na JUmaa Aweso wa CCM ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala
ya siasa, endapo watakutana katika nafasi ya ubunge upinzani utakuwa wa
aina yake.
Post a Comment