Na Mwandishi Wetu, Singida
MDAI
katika Kesi ya madai ya talaka Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa
Shule ya St. Mathew, Thadei Mtembei amehoji uhalali wa mahakama kufikia
kukagua mali zake siku ya Jumamosi bila kupitia mahakama yoyote hapa
Singida.
Kesi
hiyo ambayo inasikilizwa mahakama ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar
es Salaam, juzi (Jumamosi) ililazimika kuhamia mkoani Singida baada ya
mdaiwa (Thadei Mtembei) kuitaka mahakama kuhamia mkoani Singida kwa
gharama zake ili kuhakiki nyumba ambazo alidai alimjengea Mwangu.
Mtembei katika hoja yake ya kuitaka mahakama kuhamia Singida alisema yuko tayari kulipa gharama zote ikiwemo nauli na posho.
Hakimu
anayesikiliza kesi hiyo Rajab Tamaambele, na wakili wa Mtembei ambaye
ni mtoto wa mke mkubwa wa Mtembei (Peter Mtembei), karani na kesi na
mtumishi wa mahakama ni miongoni mwa watu waliofika kwa ajili ya ukaguzi
na uhakiki wa nyumba hizo.
Hata
hivyo hakukuwepo na wazee wa baraza jmbo ambalo mwangu pia
alililalamikia. Mwangu alidai kuwa licha ya kuwa hafahamu sheria
kutokana na kutokuwa na elimu hata ya Sekondari lakini kitendo cha
mahakama kufika Jumamosi kwa ajili ya kufanya uhakiki na ukaguzi haioni
kama ni ha haki na pia kulikuwa hakuna afisa ustawi wa jamii.
Alidai hakimu kuongozana na wakili wa kesi hiyo na kuwa pamoja muda wote haoni kama atatendewa haki katika shauri hilo.
“Mimi
nahoji ushirikiano huu kama utanitendea haki kwani watu wametoka pamoja
Dar es Salaam wameongozana kwenye magari binafsi nafika eneo la tukio
nakuta msafara wa hakimu, wakili wa mdaiwa, mwenyekiti wa kitongoji
ukiwa umeshafika mbele ya nyumba ambayo walitaka kuanza kuihakiki”
alidai.
Alidai
hata Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Mahamoud alisema hajapewa taarifa
yoyote ya maandishi kwani alishtukizwa na kupelekwa kwenye nyumba hiyo
ambayo alisema hafahamu kama ni ya Mwangu.
Pia
alihoji uhalali wa mtoto wa Mtembei ambaye ni wakili kusimamia shauri
hilo katika mahakama ya Mwanzo huku mara kadhaa akimtolea maneno ya
kashfa kama ni mfunga vidonda tu hawezi kujenga nyumba.
Mwangu
alisema alishawahi kuiambia mahakama kuwa nyumba zake za Singida
alizijenga na aliamua kuziuza kwa ajili ya elimu ya watoto wake ambao
walitelekezwa na baba yao lakini cha kushangaza mahakama kwa amri ya
Mtembei ikataka kufika Singida kuhakiki nyumba zake.
Hata
hivyo mahakama ilikagua nyumba tatu ambapo moja ilikuwa imeshauzwa kwa
Sh. Milioni 15 na nyingine iliuzwa ikiwa katika hatua ya msingi.
Baada
ya kumalizika kwa uhakiki huo hakimu Tamaambele alimtaka Mwangu
kuhakikisha anawasilisha mahakamani nyaraka zote za nyumba na kuwapeleka
watoto mahakamani kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu Agosti 25, mwaka
huu.
Post a Comment