WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza na wadau na viongozi wa Maeneo ya Jumuia ya Hifadhi ya Wanyamapori nchini (WMA), ulioanza jana jijini Arusha kujadili uboreshaji mfumo wa usimamizi na uendeshaji jumuia hizo. |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi
yasiyozingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi
yamekua tishio kwa maeneo uhifadhi
hivyo kupelekea uvamizi wa maeneo hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na
kilimo kinyume cha utaratibu.
Nyalandu
amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kati ya Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori
(WMAs) uliofanyika jijini hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu utakaorithiwa na vizazi vijavyo mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi
kuzingatiwa.
Waziri huyo
amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi
za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi hivyo amewataka wadau wa utalii
kugawanya uwekekezaji kwa kuwekeza nje
ya hifadhi.
“Mtu
anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu vizuri lazima tutawanye uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi”
Alisema Nyalandu
Alisema kuwa
kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo
ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya nyingine 17 ziko katika hatua mbalimbali za
uanzishwaji,amezitaka jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi
katika kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanayama pori ya mwaka
1998.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard Chambulo alisema kuwa ili uhifadhi uweze
kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na hati miliki za maliasili ili waweze
kuzitunza vyema.
Chambulo
anaeleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni nguzo muhimu sana
kwa uhifadhi itakayosaidia kuwa na
utalii endelevu kwa vizazi na vizazi.
Post a Comment