Aliyesimama
ni Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini,
yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda
akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha juu ya kushuka kwa
ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema
na miziki hafifu isiyoweza kustahimili ushindani wa soko la kazi za
burudani duniani anayefatia ni katibu wa shirika hilo Frank Martin
,watatu ni James Mollel katibu tawi laArusha pamoja na Gabriel Simbeye
mjumbe(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
katibu
wa shirika la Tanzania Audio Visual Works Distributors Frank
Martin amebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa na
mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa
zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development
International ya 2011.
Mwandishi wa habari kutoka Daily News Marc Nkwame akiuliza swali
Ramadhani Mvungi mwakilishi wa starTV Arusha akifuatilia jambo katika kamera yake siku hiyo
Muonekano ndani ya ukumbi
Msanii mkongwe wa filamu hapa Nchini,
Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’ akizungumzia hali halisi ya kushuka
kwa soko la sanaa hapa Nnchini ambapo alisema kuwa hata kampuni za
usambazaji filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa kuwapa waandaaji
malipo finyu
Mmiliki wa Jamiiblog Pamela Mollel akishow love na Msanii mkongwe wa filamu, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado
Muziki
na Filamu zinazorekodiwa nchini zinadaiwa kupoteza umaarufu nchini
kiasi cha kusababisha soko lake kuangukia pua, huku waandaaji na
wasambazaji wake wengi wakiamua kujitoa na kutafuta shughuli zingine za
kufanya.
Mwenyekiti
wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani
‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda, pamoja na
katibu wa shirika hilo Frank Martin wamelaumu kushuka kwa ubunifu
miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki
hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani
duniani.
“Tathmini
kutoka wasambazaji waliochini ya ‘Tanzania Audio Visual Works
Distributors,’ ambao wanafikia 200 kwa sasa, imeonesha kupungua kwa kazi
za Sanaa yaani muziki na filamu kwa asilimia Zaidi ya 50 na hii
imesababishwa na kukosekana kwa masoko ya kazi hizo nchini,” alisema
Katibu wa chama hicho, Frank Martini.
Wakizungumza
jijini hapa wakati wa kikao maalum kati ya wasambazaji na wasanii,
viongozi hao wamebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa
na mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa
zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development
International ya 2011.
“Kipindi
hicho tulishihudia filamu mpya takriban 10 zikitolewa kila wiki, lakini
hali ni tofauti kwa sasa ambapo tunashuhudia chini ya filamu 10 kwa
mwezi mzima huku idadi hiyo kwa mwaka ikiwa ni wastani au chini ya
sinema 120 tu hii ni kwa mujibu wa rekodi ya wasambazaji wa kazi za
Sanaa nchini kwa mwaka huu wa 2015,” aliongeza Martini.
“Wasambazaji
na waandaaji (producers) wa sinema na muziki wameamua kujitoa kwenye
tasnia hii na kutafuta shughuli mbadala za kufanya,” alisema mwenyekiti
wa taasisi hiyo Baraka Nyanda.
Wakizungumzia
muziki wamesema eneo hili ndilo limeathirika Zaidi kwa sababu watu
hawanunui tena nyimbo zilizorekodiwa kwenye santuri za CD ambazo ndizo
chanzo kikuu cha mapato kwa wasanii na wasambazaji.
“Wasanii
wengi wa muziki wamekuwa wakisambaza kazi zao kupitia mitandao kama
You-Tube ambako mashabiki wao huzipakua bure, wengine huthubutu hata
kugawa CD za nyimbo zao mpya bure kabisa mitaani alimradi kujenga jina
tu huku wasambazaji wakikosa kipato,” walisema wasambazaji hao.
Msanii
mkongwe wa filamu, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’ amesema kuwa
hata kampuni za usambazaji filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa
kuwapa waandaaji malipo finyu; “Hawa wananunua master ya sinema moja
mpya kwa shilingi milioni 10 tu, ambazo utakuta ndio gharama za
ktengenezea filamu sasa hapo unabaki na nini?” aliuliza.
Kwa
mujibu wa Rado, maadam wasambazaji wameamua kiwango cha kununua sinema
mpya ni milioni 10, basi watengenezaji huamua kulipua kazi zao kwa
kuwatumia waigizaji rahisi na maprodyuza kwa kuokoteza alimradi tu
kupunguza gharama za uandaaji ili mwisho wa siku wapate faida.
Lakini
kwa mwenzake, Hussein Rajab Usichonge, tatizo ni kwamba wasanii
chipukizi hawathaminiwi na matokeo yake tasnia inakosa vitu vipya; “Wao
wanaangalia ma-super star tu, ingawa wengi wamechoka na wamekosa
ubunifu, sisi chipukizi ndio tungeleta mabadiliko lakini tunabaniwa,”
alisema.
Post a Comment