PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MFANYABIASHARA LENGANASI MDELE AWEZESHA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 54 KUJENGA VISIMA VYA MAJI WILAYANI SIMANJIRO.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Lenganas   Mdele akizungumza na wananchi  katika harambee ya kuchangia ujenzi wa visima vya maji na matanki kwa wananchi wa kata za Naraka...
Lenganas  Mdele akizungumza na wananchi  katika harambee ya kuchangia ujenzi wa visima vya maji na matanki kwa wananchi wa kata za Narakawo na Lobosiret   zilizopo  wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyaraambapo jumla ya shilingi milioni 54 ilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika jana katika kata ya Lobosiret


Lenganas  Mdele akizungumza na wananchi  katika harambee ya kuchangia ujenzi wa visima vya maji na matanki kwa wananchi wa kata za Narakawo na Lobosiret   zilizopo  wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara ambapo alikua mgeni wa heshima.jumla ya shilingi milioni 54 ilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika jana katika kata ya Lobosiret.Picha na Ferdinand Shayo 



Wananchi wa kata za Narakawo na Lobosiret  cha zilizopo  wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara wamefanya Harambee na kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 58 zitakazosaidia kujenga kisima cha maji pamoja na matanki ya kuhifadhia maji  kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo yao hasa katika kipindi cha kiangazi ambacho hugubikwa na uhaba wa maji.

Akizungumza katika Harambee hiyo Mgeni rasmi Lenganas  Mdele ambaye ni Mfanyabiashara  alisema kuwa wanakijiji hao hutembea umbali mrefu kilomita 30 wakitafuta maji na kutumia masaa 9 hivyo kushindwa kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi hali inayoathiri maendeleo ya jamii hiyo hususani kinamama wa jamii ya wamasai.

“Tumeona haja ya kuunganisha nguvu kama wananchi kwa kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa matanki ya kuhifadhia maji yatakayowasaidia wananchi na kutatua kero ya maji inayowakabili kwa muda mrefu ,baada ya harambee hii ujenzi utaanza  mapema wiki hii” Alisema Lenganas

Mzee wa Kimila wa jamii ya Wamasai  Ezekiel Lesenga   ameiomba serikali ijitokeze kuwaunga mkono katika juhudi zao kwani watu wa vijijini wamekua wakisahaulika katika masuala mbalimbali hususani huduma za kijamii kama vile maji,hospitali na shule.

Kwa upande wao Wanakijiji Maria Edward na Natanamwaki wamesema kuwa wamekua wakipata shida ya maji na kulazimika kutumia maji ya bwawani ambayo hushirikiana na mifugo kuyatumia hivyo kupata magonjwa ya kuhara,homa ya matumbo  pamoja na Typhod.


Mtendaji wa kata ya Narakawo  Meshack Tureto  alisema kuwa kijiji hicho kinachokadiriwa kuwa na idadi ya watu 2000 na mifugo 6000 kinakabiliwa  uhaba mkubwa wa maji hivyo ameiomba serikali ichukue hatua za haraka kusaidia kutatua tatizo hilo kwa kushirikiana na wananchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top