Na Ferdinand Shayo,Karatu
Wananchi wa kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilaya ya
Karatu mkoani Arusha wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya
hali inayowalazimu kutembea umbali wa kilomita 40 kufuata huduma hiyo muhimu.
Aidha wamekuwa wakikumbwa na adha kubwa hasa kwa kina mama
wajawazito wanapokwenda kujifungua hali iliyowapelekea wananchi hao kuunganisha nguvu na kujenga kituo cha afya
kitakachowasogezea huduma za afya Karibu.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho akisoma taaarifa ya utekelezaji
wa mradi huo mbele ya Uongozi wa Kampuni ya bia ya TBL iliyofika kijijini hapo
na kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye gharama ya shilingi milioni 22 ili
kusaidia wodi ya uzazi na watoto ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono
shughuli za kijamii.
Amesema kuwa baada ya kukabiliwa na changamoto hiyo kwa muda
mrefu wananchi waliamua kujenga kituo chicho cha afya kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Ngorongoro na kwa sasa wako katika umaliziaji wa nyumba za wauguzi
pamoja na kuweka vifaa mbali mbali hivyo ameishukuru TBL kwa msaada huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya TBL ,Robin
Goetzsche na Afisa Mahusiano Doris
Malulu wamesema kuwa wameguswa kuisaidia jamii hiyo kutokana na mwamko wao wa
kulima shahiri na kuonyesha nia ya kutumia fedha wanazozipata kujiletea
maendeleo hivyo kuwa mfano wa kuigwa kwa
wakulima wote wa Shahiri nchini kote.
Wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba huishi kwa kutegemea
kilimo cha shayiri ambayo wanaiuza kwa kampuni ya TBL na kujipatia kipato
kinachowawezesha kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Post a Comment