PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mume auza ardhi na kwenda kuoa mke mwingine akimuacha wa awali katika mateso
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Unyanyasaji wa kina mama, bado ni janga kubwa sana katika nchi yetu. Kuanzia vipigo, hadi kutekelezwa, kutumikishwa kama chombo cha u...

Unyanyasaji wa kina mama, bado ni janga kubwa sana katika nchi yetu. Kuanzia vipigo, hadi kutekelezwa, kutumikishwa kama chombo cha udhalilishaji mali tu katika familia, hadi kutumika kama chombo cha starehe, haya ni baadhi tu ya madhila ambayo kina mama wamekuwa wakikumbana nayo karibu kila siku, licha ya elimu ambayo imekuwa ikitolewa kuhusu usawa wa kijinsia.

Neema Awaki, ni miongoni mwa kinamama ambao kadhia hii ya maisha imewakumba. Si tu kwamba mama huyu, mkazi wa kijiji cha Aya Naaday, ametelekezwa na mumewe, bali pia ameachwa katika mazingira magumu baada ya mtu huyo, anayeelezwa kuwa alikuwa mumewe, kuuza ardhi waliyokuwa wanaimiliki kwa pamoja, kabla ya kutokomea mahali pengine, ambako anaelezwa kuwa anayafurahia maisha akiwa na mwanamke mwingine
 pmt ilimtembelea mama huyu, baada ya kupata taarifa ya jinsi anavyo teseka kutoka kwa wasamaria wema. Na hapa, ni simulizi kamili kuhusu mama huyu.

Hata hivyo, hakuna marefu yasiyo na ncha. Hatimaye mwisho wa mateso ya mama huyo na wanawe umekuja baada ya juhudi za kuipaza sauti hii iliyokuwa imefichika, kufanikiwa kuwezesha kupatikana kwa jibu la kitendawili hiki.
Lakini je, ni wanyonge wangapi wanaishi katika hali kama hii? Na ni lini watadumu katika mateso ya namna hii?

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top