. Vitambulisho kutolewa kwa wenye stashaada au shaada.
. Wakajanja watajwa kudhalilisha nchi katika mataifa mengine.
Kubadilika kwa teknolojia na hali halisi
ya maisha, kumebadilisha tasnia ya habari hivyo kuwalazimu waadishi wa
habari wabadilike kulingana na hali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa mjini
Dodoma, mkurugenzi wa habari maelezo Bwana Assah Mwambene, amesema kuwa
wanahabari waende sambamba na wanaowahabarisha kwa kuwapa habari zilizo
sahihi na zenye kuleta mabadiliko.
Bwana Mwambene amefafanua kuwa matumizi
ya mtandao kihabari yanakuwa makubwa zaidi kwasasa, huku akiongeza kuwa
kuna kila sababu ya kuweka utaratibu maalumu kuwezesha watumiaji kuweka
habari zenye tija kwani watakuwa wakifuatiliwa na kusimamiwa na mamlaka.
Amesema ukishakuwa mwanahabari,
unatakiwa kuchambua mambo mambo buhimu kuwekwa kwenye chombo husika, kwa
kuvaa viatu vya yule anayeandikwa au kutangazwa kama umemtendea vyema
au vibaya, huku akitolea mfano picha za utupu na sura za watu
zinazowekwa na baadhi ya wamiliki wa mitandao kwa udhalilishaji.
Amesisitiza kuwa Tanzania imekuwa na
baadhi ya wadau wanaojidhalilisha na kuingiza mijada kati ya Tanzania na
mataifa mengine, kwasababu ya watanzania kubeza mambo yaliyopo nchini
badala ya kutafuta jinsi ya kurekebisha.
Hatahivyo Bwana Mwambene, amepongeza
uanzishaji wa chombo cha SAUTI kinachomiliki mtandao wa
sautiyamnyonge.com, akisema kuwa inaweza kuwa chachu ya mabadiliko
nchini, huku akiomba TMF isaidie kuwakutanisha wanahabari na maafisa
habari nchini, kujadili jinsi ya waandishi kupata habari na jinsi
maafisa kutoa habari.
Waandishi habari 20 kutoka kanda
mbalimbali wanaounda mtandao wa SAUTI, wanaendelea na mafunzo ya
kuandika na kutangaza habari kupitia mtandao, yaliyodhaminiwa na mfuko
wa waandishi wa habari Tanzania TMF, ambapo pia wanajadili jinsi ya
uendelezaji wa taasisi ya SAUTI kwa lengo la kuwafikia wanyonge na
kuleta sauti zao adharani.