PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Kubadilika kwa matumizi ya mtandao kwa walazimu wanahabri kubadilika.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Dodoma . Vitambulisho kutolewa kwa wenye stashaada au shaada. . Wakajanja watajwa kudhalilisha nc...


 
Kubadilika kwa matumizi ya mtandao kwa walazimu wanahabri kubadilika.
Dodoma

. Vitambulisho kutolewa kwa wenye stashaada au shaada. . Wakajanja watajwa kudhalilisha nchi katika mataifa mengine.
Kubadilika kwa teknolojia na hali halisi ya maisha, kumebadilisha tasnia ya habari hivyo kuwalazimu waadishi wa habari wabadilike kulingana na hali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa mjini Dodoma, mkurugenzi wa habari maelezo Bwana Assah Mwambene, amesema kuwa wanahabari waende sambamba na wanaowahabarisha kwa kuwapa habari zilizo sahihi na zenye kuleta mabadiliko.
Bwana Mwambene amefafanua kuwa matumizi ya mtandao kihabari yanakuwa makubwa zaidi kwasasa, huku akiongeza kuwa kuna kila sababu ya kuweka utaratibu maalumu kuwezesha watumiaji kuweka habari zenye tija kwani watakuwa wakifuatiliwa na kusimamiwa na mamlaka.
Amesema ukishakuwa mwanahabari, unatakiwa kuchambua mambo mambo buhimu kuwekwa kwenye chombo husika, kwa kuvaa viatu vya yule anayeandikwa au kutangazwa kama umemtendea vyema au vibaya, huku akitolea mfano picha za utupu na sura za watu zinazowekwa na baadhi ya wamiliki wa mitandao kwa udhalilishaji.
Amesisitiza kuwa Tanzania imekuwa na baadhi ya wadau wanaojidhalilisha na kuingiza mijada kati ya Tanzania na mataifa mengine, kwasababu ya watanzania kubeza mambo yaliyopo nchini badala ya kutafuta jinsi ya kurekebisha.
Hatahivyo Bwana Mwambene, amepongeza uanzishaji wa chombo cha SAUTI kinachomiliki mtandao wa sautiyamnyonge.com, akisema kuwa inaweza kuwa chachu ya mabadiliko nchini, huku akiomba TMF isaidie kuwakutanisha wanahabari na maafisa habari nchini, kujadili jinsi ya waandishi kupata habari na jinsi maafisa kutoa habari.
Waandishi habari 20 kutoka kanda mbalimbali wanaounda mtandao wa SAUTI, wanaendelea na mafunzo ya kuandika na kutangaza habari kupitia mtandao, yaliyodhaminiwa na mfuko wa waandishi wa habari Tanzania TMF, ambapo pia wanajadili jinsi ya uendelezaji wa taasisi ya SAUTI kwa lengo la kuwafikia wanyonge na kuleta sauti zao adharani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top