Unyanyasaji
wa kina mama, bado ni janga kubwa sana katika nchi yetu. Kuanzia
vipigo, hadi kutekelezwa, kutumikishwa kama chombo cha udhalilishaji mali
tu katika familia, hadi kutumika kama chombo cha starehe, haya ni baadhi
tu ya madhila ambayo kina mama wamekuwa wakikumbana nayo karibu kila
siku, licha ya elimu ambayo imekuwa ikitolewa kuhusu usawa wa kijinsia.
Neema Awaki, ni miongoni mwa kinamama
ambao kadhia hii ya maisha imewakumba. Si tu kwamba mama huyu, mkazi wa
kijiji cha Aya Naaday, ametelekezwa na mumewe, bali pia ameachwa katika
mazingira magumu baada ya mtu huyo, anayeelezwa kuwa alikuwa mumewe,
kuuza ardhi waliyokuwa wanaimiliki kwa pamoja, kabla ya kutokomea mahali
pengine, ambako anaelezwa kuwa anayafurahia maisha akiwa na mwanamke
mwingine
pmt ilimtembelea mama
huyu, baada ya kupata taarifa ya jinsi anavyo teseka kutoka kwa
wasamaria wema. Na hapa, ni simulizi kamili kuhusu mama huyu.
Hata hivyo, hakuna marefu yasiyo na
ncha. Hatimaye mwisho wa mateso ya mama huyo na wanawe umekuja baada ya
juhudi za kuipaza sauti hii iliyokuwa imefichika, kufanikiwa kuwezesha
kupatikana kwa jibu la kitendawili hiki.
Lakini je, ni wanyonge wangapi wanaishi katika hali kama hii? Na ni lini watadumu katika mateso ya namna hii?
Post a Comment