Mhe.
Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa
Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada
Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya
Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)Wajumbe
wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo
pichani.)
Rais
Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo
pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi kuwathamini Watanzania
waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya
maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora.
Mhe. Rais Kikwete akiteta jambo na Waziri Membe kabla ya kuwahutubia MabaloziWaziri
Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi
Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi
wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi Mhe. Rais Kikwete akiongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.
Mhe. Rais
Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue, Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge, Mhe. Mussa Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul
Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote.
Mhe. Rais Kikwete na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake.
Mhe. Rais
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Post a Comment