Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Watoto wa mitaani wanaoishi jijini Arusha katika mazingira hatarishi
wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata
sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.
Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya
watoto wa mitaani jijini Arusha,Sawale Maghema amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto wa
mitaani kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika
vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.
Sawale alisema kuwa iwapo watoto wa mitaani watatelekezwa na
jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania
hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .
“Watoto wa mitaani tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na
kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili
kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel
litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika
wataendelea kuwa na maisha mabaya” Alisema Sawale
Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa Panju alijitolea kuwasaidia watoto wa mitaani kwa
kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa watoto hao ili waweze kupata
mahitaji muhimu ,Ameeleza kuwa jamii
inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa
kwenye mazingira hatarishi.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha ,Hassan Omari
akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wa mitaani wana
ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika
mbali na kulisaidia taifa .
“Maisha ya baadae yanawategemea watoto wa sasa ambao ndio
sisi watoto wa mitaani juhudi zikiimarishwa wanaweza kuchangia maendeleo kwa
taifa letu” Alisema Hassan
Post a Comment