PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Lukuvi Aagiza Upimaji ardhi na upangaji wa miji
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Na Ferdinand Shayo,Longido Waziri wa Ardhi nyumba na makazi Wiliam Lukuvi ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Longido kuh...

 

Na Ferdinand Shayo,Longido

Waziri wa Ardhi nyumba na makazi Wiliam Lukuvi ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Longido kuhakikisha kuwa wanapima ardhi pamoja na kupanga miji ili kuepukana na tatizo la ujenzi holela .
Aidha amesema kuwa miji inayokua inapaswa ipangwe mapema ili kuepushwa suala la bomoa bomoa ambalo hujitokeza baadae na kuzua migogoro.
Lukuvi ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa mradi nyumba za watu wenye kipato cha chini na  cha kati unaotekelezwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) katika wilaya ya Longido na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 921.Lukuvi amewaasa wakazi wa longido kuchangamkia fursa hiyo ya kununua nyumba hizo bora kwa makazi ya watu.

Mkurugenzi wa shirika la nyumba Nehemia Mchechu amesema kuwa mradi huo utawawezesha wakazi wa Longido kuwa na makazi bora na kumiliki nyumba zao wenyewe hivyo ametoa wito kwa wakazi wa Longido kujitokeza kununua nyumba hizo kwa bei nafuu.

Mbunge wa Longido Lekule Laizer amesema kuwa hitaji la makazi bora kwa jamii ya wafugaji litafikiwa na mradi huo hivyo amewashauri wafugaji kumiliki nyumba ili kujipatia heshima kwani haiwezekani kuwa na maisha bila nyumba.
Katika Ziara hiyo Waziri Lukuvi amewaagiza viongozi wa mila pamoja na viongozi wa kiserikali kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Longido ,Monduli na Wilaya ya Arusha ili kuepuka migogoro mbali mbali inayojitokeza na kuathiri shughuli za kijamii.
Kwa upande wake Katibu tawala msaidizi ,miundombinu Hamdun Mansour amesema kuwa migogoro mingi ya ardhi ni kati ya wananchi wenyewe pamoja na ile inayohusisha wawekezaji na wananchi ,Mkoa umekua ukifanya juhudi za kutatua migogoro hiyo ambayo wakati mwingine huathiri hali ya amani.
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo imekua ikiathiri amani na utulivu pamoja na shughuli za maendeleo,utatuaji wa migogoro hiyo utaleta tija kwa maendeleo na kudumisha amani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top