PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KISWAHILI KUTUMIKA KATIKA SHUGHULI MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Raisi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani Akihutubia  mkutano wa Haki za binadamu uliofanyika jana  jijini...
Raisi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani Akihutubia  mkutano wa Haki za binadamu uliofanyika jana  jijini Arusha lengo la kuimarisha haki za binadamu na kushirikisha taasisi binafsi na za serikali katika kuisaidia Mahakama hiyo .Picha na Ferdinand Shayo   


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Raisi wa Mahakama ya Afrika  ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani amesema kuwa lugha ya Kiswahili itaanza kutumika katika mahakama hiyo ili kuwawezesha watu kusoma na kuelewa taarifa muhimu zinazotolewa  zitakazowawezesha kujua na kuimarisha haki hizo za msingi kwa kila mmoja
.
Jaji Agustino Ramadhani amesema kuwa lugha ya Kiswahili inazungumzwa na nchi nyingi barani Afrika hivyo umefika wakati wa kubadilisha taarifa na nyaraka mbali mbali kutoka lugha za kigeni  na kuwa katika Kiswahili ili kukuza uelewa wa watu juu ya haki za binadamu.

Raisi huyo ameeleza hayo katika mkutano wa haki za binadamu ulioandaliwa na Mahakama hiyo kwa kushirikiana na Mashirika na taasisi binafsi zinazojihusisha na haki za binadamu uliofanyika jijini Arusha jana,Ramadhani amesema kuwa mashirika binafsi yana nafasi kubwa ya kutoa elimu  kwa wananchi na kuhamasisha uzingatiaji wa haki hizo.

Mwenyekiti wa Mashirika binafsi yanayotetea haki za binadamu na kufanya kazi kuisaidia mahakama hiyo George Kisoro  amesema kuwa suala la kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya Makosa ya jinai kwa mujibu wa mkataba wa Malabo  unaojulikana kama Malabo Protocol na kupitishwa Juni 2014 bado una kasoro mojawapo ni kuwepo kwa kifungu ambacho hakiruhusu rahisi kushitakiwa akiwa katika kipindi cha uongozi wake.

“Kifungu hichi kitawafanya viongozi wa Afrika kung`ang`ania madaraka kwa kuogopa kuwa iwapo wakiachia madaraka watashitakiwa katika mahakama hiyo kwa upande mwingine ina madhaifu”  Alisema George

George alisema kuwa kutokana na Viongozi wa Afrika kutorishiwa na mwenendo wa Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai iliyoko  the Heague walipendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Afrika ya makosa ya jinai itakayoendesha makosa ya jinai yanayowakabili viongozi.

Anaeleza kuwa kwa sasa hali ya haki za binadamu kwa bara la Afrika bado ni mbaya hasa katika maeneo yenye vita kama nchini Congo na Sudan ambako vitendo vya kikatili na unyanyasaji wanafanyiwa wanawake na watoto ikiwemo ubakaji,kukatwa viungo vya mwili,vipigo vikali  .Katika maeneo hayo kuuana imekua ni utamaduni wa kudumu suala ambalo si zuri.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top