PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YAWATAKA WASOMI KUWA WABUNIFU ILI KUJIAJIRI NA KUTOA AJIRA KWA WATANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Na Ferdinand Shayo,Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Felix Ntibenda amewaasa wahitimu wa vyuo  kuwa wabunifu na kutumia elimu waliyon...

 

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Felix Ntibenda amewaasa wahitimu wa vyuo  kuwa
wabunifu na kutumia elimu waliyonayo kujiajiri badala kusubiri
kuajiriwa serikalini.

Akizungumza katika mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu Huria tawi la Arusha
amesema kuwa kutokana ongezeko kubwa la wahitimu kila kukicha serikali
inashindwa kuwaajiri hasa ukizingatia ufinyu wa  nafasi chache
zilizoko serikalini.


Mshauri wa Chuo hicho ambaye pia aliwahi kuwa Mshauri wa Baba wa Taifa
Mwalimu Nyerere  ,Samueli Kasori ameishauri serikali iwatumie vizuri
wataalamu wazawa kukuza ustawi wa jamii na taifa badala ya kuwaacha na kutowajali hali inayowapelekea kutimikia nchi za nje na kuwanufaisha wageni .

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo hicho John Msindai amesema kuwa chuo
kikuu hicho huria kinatoa fursa kwa watanzania kujiendeleza kielimu na
kubadilisha maisha yao kupitia maarifa wanayoyapata.

Katibu wa Chama cha Wanafunzi kituo cha Arusha Kassimu Mfinanga
amesema kuwa changamoto zinazowakabili wanafunzi hao ni pamoja na
uhaba wa fedha,baadhi ya  waajiri kutowaruhusu wafanyakazi wao
kujiendeleza.

Kwa upande wao Wahitimu Andrea Ngobole aliyechukua shahada ya uandishi wa habari  amesema kuwa elimu walitoipata
itawasaidia kuibadilisha jamii na kuwa chachu ya maendeleo.

Jumla ya Wahitimu 55 wamehitimisha masomo yao kwa taaluma za Sheria,Uhasibu,Habari .changamoto kubwa ikiwa
ni ajira na nmna elimu yao itanufaisha jamii na taifa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top