Mwaka mmoja kabla ya kiongozi wa
taifa la North Korea Kim Jong Un kuchukua mamlaka agizo lilitolewa kwa
mtu yeyote aliye na jina kama lake kulibadilisha ili kuendeleza
utamaduni wa utawala wa familia ya Kim.
Kulingana na nakala za
kimataifa zilizopatikana na Runinga ya KBS nchini Korea Kusini zilizo na
maagizo ya utawala wa Kim Jong wa Pili vitengo vya polisi na jeshi
vilitakiwa kuhakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa.
Agizo hilo lilitolewa mnamo mwezi January mwaka 2011 mda mfupi baada ya Kim Jong Un kuteuliwa kama mrithi wa babaake.
Kim Jong wa Pili alifariki mwezi Disemba mwaka huohuo.
''Vitengo
vyote vya chama na mamlaka ya usalama ni sharti viweke orodha ya watu
walio na majina ya Kim Jong Un na kuwafundisha vile watakavyobadilisha
majina yao'',ilisema nakala hiyo ambayo baadhi yake ilitangazwa moja kwa
moja na runinga ya KBS.
Mpango huo ulishirikisha kubadilisha
majina katika stakhabadhi rasmi,ikiwemo katika kadi za usalama wa jamii
na vyeti vya masomo.
Maafisa pia waliagizwa kukataa vyeti vya kuzaliwa vya watoto wachanga walio na majina ya Kim Jong Un.
Vilevile Mamlaka ziliagizwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayelalamika ama kueneza uvumi.
Chimbuko la agizo hilo rasmi halikuweza kuthibitishwa huku wizara ya Seoul ikikataa kuthibitisha iwapo madai hayo ni ya ukweli.
Lakini
Afisa mmoja wa utawala wa Pyong yang alidai kwamba Utawala huo
uliwapiga marufuku raia wake kutumia jina la rais wa kwanza wa taifa
hilo Kim wa pili Sung na mwanawe Kim jong wa Pili.
Post a Comment