Na Ferdinand Shayo, Arusha.
Watanzania wameshauriwa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya
zao na kujikinga na magonjwa nyemelezi pamoja na kukabiliana na mazingira
hatarishi.
Mwalimu wa klabu ya Taekwondo ya AICC iliyoko jijini Arusha
David Samson amesema hayo jana wakati wa mazoezi ya klabu hiyo na kuongeza kuwa
utamaduni wa kufanya mazoezi unaulinda mwili dhidi ya hatari ya kupata magonjwa
.
Wanachama wa klabu hiyo Betty Senny na Kelvin Gasper ambaye alihitimu mafunzo ya
stashahada ya Taekwondo wameeleza manufaa wanayoyapata kwa kufanya mazoezi ni
kujikinga na magonjwa hatarishi.
Jenny Senny ni Mwanachama anasema kuwa mazoezi wanayoyafanya
yanawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na kuepuka magonjwa .
Utamaduni wa kufanya mazoezi ni muhimu kwa watanzania kwani
unawasaidia kuepuka magonjwa,kuchangamsha mwili na akili .
Post a Comment