PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MWANAFUNZI WA UDAKTARI AJIFUNGUA NA KUMTUPA MTOTO KATIKA PIPA LA UCHAFU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mtoto aliyetupwa na mwanafunzi wa udaktari akiwa anaapata matibabu katika hospitai ya KCMC picha hii ni kwa mujibu mdau aliyeitu...
Mtoto aliyetupwa na mwanafunzi wa udaktari akiwa anaapata matibabu katika hospitai ya KCMC picha hii ni kwa mujibu mdau aliyeituma katika mtandao wa instargram


NA: EDNA BONDO
 

MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza shule ya viungo KCMC mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro, Rachel Malima (22), amewekwa chini ya uangalizi maalumu wa madaktari baada ya kujifungua na kumtelekeza mtoto kwenye pipa la kuhifadhia takataka katika vyoo vya hospitali hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Ofisa Uhusiano wa hospitali ya KCMC, Gabriel Chiseo, alikiri kutokea kwa tukio hilo juzi baada ya mwanafunzi huyo kushikwa uchungu wa kujifungua. 

Alibainisha kuwa, Malima alifika hospitalini hapo akiwa na wenzake na kupokelewa na wahudumu wa mapokezi na kuwekwa mapumziko wodini kabla ya muda mfupi kuomba kwenda msalani kujisaidia na kuruhusiwa.

Alieza kuwa, baada ya kufika msalani ndipo alipojifungua mtoto huyo na kumweka katika pipa la takataka na kutokomea kusikojulikana.

Inaelezwa kuwa, mara baada ya kuondoka mmoja wa wafanya usafi hospitalini hapo, aliingia msalani kwa ajili ya kuhakiki usafi na ndipo alipokuta choo kikiwa kimetapakaa damu na alipofungua pipa la takataka alikuta kichanga kikiwa na mfuko wa uzazi (Placenta), kinatupa tupa mikono na miguu na mdomoni kimesokomezwa taulo ya kike (Pad), ili sauti isisikike.
Mtoto aliyetupwa na mwanafunzi wa udaktari akiwa anaapata matibabu katika hospitai ya KCMC picha hii ni kwa mujibu mdau aliyeituma katika mtandao wa instargram

Chiseo, alisema jitihada za kumtafuta na kumkamata zilifanyika na hivi sasa yupo chini ya uangalizi maalum wa madakatari wa hospitali hiyo kwa ajili ya kumjenga kisaikolojia ili aweze kuhojiwa sababu ya kufanya hivyo.

“Hivi sasa Malima yupo chini ya uangalizi maalum, mtoto anaendelea vizuri  lakini pia bado tukio hilo halijaripotiwa polisi ila lipo chini ya kitengo cha uastawi wa jamii wa hospitali ambao watajua ni nini kitafuata baada ya Malima kupata nafuu,” alisisitiza Ofisa Habari huyo 

Kukamatwa kwa mwanafunzi huyo, kulitokana na jitihada za mashuhuda wa tukio hilo na uongozi wa KCMC, ambao walimwona Malima akiingia hospitalini hapo akiwa na baibui na alitoka akiwa anachechemea huku akiwa amesaidiwa mkoba na mtu ambaye hadi sasa hajafahamika.

credit:  Tanzania daima

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top