PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA YA UCHUMI: NGUVU YA MAAMUZI YAKO KATIKA KUBADILISHA MAISHA YAKO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. M aisha ya mtu ni matunda ya mtiririko wa maamuzi ya mtu binafsi yakiwa yamechanganyika na maamuzi y...


Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Maisha ya mtu ni matunda ya mtiririko wa maamuzi ya mtu binafsi yakiwa yamechanganyika na maamuzi ya watu wengine yanayogusa maisha yake.
Maisha uliyonayo ni matokeo ya maamuzi uliyoyafanya,nyumba uliyonayo,elimu uliyonayo,mke au mme,uchumi,biashara unayoifanya.
Uko hivyo ulivyo kutokana na maamuzi uliyoyafanya na unayoendelea kufanya ,maamuzi ya leo ni matokeo ya kesho amua vyema upate vyema.
Mafanikio yako ya kesho yanategemea maamuzi unayoyafanya leo  hivyo uamuzi unaoufanya una nguvu ya kubadilisha maisha yako.
Hakuna mtu anaweza kubadilisha maisha yako isipokuwa wewe na maamuzi yako amua kubadilika amua kufanya maamuzi sahihi upate kuishi maisha sahihi.
Kabla ya kufanya uamuzi fikiria matokeo ya maamuzi kwa mantiki hii jambo linalofanyiwa maamuzi si la kufanyiwa mzaa wala uzembe.
Watu wengi hawafanikiwi katika maisha yao kwasababu si waangalifu juu ya maamuzi  wanayoyafanya.Usifanye maamuzi ambayo yanamfurahisha mtu lakini baadae yanakusababishia majuto na uchungu.
Maamuzi yanakusaidia kufika pale unapotaka kufika ,maisha yetu ni matokeo ya maamuzi yetu .Maisha ya baade yanategemea maamuzi tunayoyafanya leo.
Kufanikiwa ni uchaguzi na kutofanikiwa pia ni uchaguzi,maisha ya mtu yanaendesha na maamuzi ama uchaguzi na si majaliwa wala bahati nasibu wala bahati mbaya,kama zipo ni nadra sana ila zaidi ya asilimia 90% ya maisha yetu yanatokana na maamuzi yetu.
Maamuzi unayoyafanya  yanaweza kwenda kwa watoto,wajukuu na vitukuu, vizazi na vizazi vijavyo vinaweza kunufaika na maamuzi yako ama kuathiriwa kwa maana ya kupata madhara.
Kila siku binadamu anafanya maamuzi ,hivyo maamuzi ni kitu ambacho hakiepukiki ,hakikwepeki ,maisha yanatuweka njia panda mara kwa mara na kututaka tuchague.
Watu wengi wanakosa utulivu wa ndani wa kufanya maamuzi wanajikuta wanafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kuishi maisha ambayo si sahihi.
Maamuzi yako yanaweza kubadilisha mustakabali wa maisha yako ,hivyo usiuchekee uamuzi utakaokupa majuto baadae,utakao kubakiza kwenye umasikini na matatizo uliyonayo.
Maaumuzi ni gharama ya kulipia maisha,kama kuna mambo unayahitaji kwenye maisha yako yanaweza kubakia kua ndoto au kwenye mawazo mapaka utakapoamua kuyatoa kwenye uhalisia na kujimilikisha.
Fanya maamuzi sahihi uapate maisha sahihi.
0765938008



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top