Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari
akizungumza na wenyeviti wapya wa mtaa pamoja na wajumbe waliochaguliwa
kwa tiketi ya CHADEMA katika Wilaya ya Arumeru Mashariki katika semina
iliyoandaliwa na Mbunge huyo ya kuwahamasisha kuwatumikia wananchi
ilifanyika katika ukumbi wa usariver academy leo.Picha na Ferdinand
Shayo
Mbunge wa
Arumeru Mashariki Joshua Nassari amewataka wenyeviti wapya wa mitaa waliochaguliwa kwa tiketi ya
Chadema kutojihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu katika kipindi cha
uongozi wao na kusisitiza kuwa chadema sio sehemu ya kupiga dili.
Aidha
amewaasa Wenyeviti hao kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya haki kutokana na
dhamana kubwa waliyopewa na wananchi hivyo wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa
uongozi na uwajibikaji.
Nassari
Akizungumza katika semina ya siku mbili ya Wenyeviti hao na wajumbe yenye lengo
la kuhamasisha ufanisi na utendaji kazi wa viongozi hao wapya kabla ya kuingia
kazini amesema kuwa wanakwenda kuwatumikia wananchi bila kuwabagua .
“Mmechaguliwa
maana yake ni kurudisha tumaini kwa Watanzania ,wananchi waone tofauti sio tofauti ya kubadilisha bendera na kuweka
bendera zenu bali kuwajibika” Alisema Nassari
“Wenyeviti
wa mitaa mnapaswa kujua kuwa mbeba dhamana ya watu wengi mikononi mwenu hivyo
mnapaswa kuitendea kazi” Nassari
Mwenyekiti
wa CHADEMA wilaya ya Meru Gadieli Mwanda amewataka Wenyeviti hao kujiandaa
kufanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi ,utumishi ambao hauko ndani ya CCM.
Katibu wa
CHADEMA wilaya Stephano Mungure anaeleza kuwa ushindi walioupata katika vijiji
32 unazidi kukifanya chama hicho kuwa tumaini la wananchi sifa ambayo inatakiwa
iendelezwe na viongozi hao.
|
Post a Comment