PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA YA UCHUMI: MAISHA NI USHINDANI UMEJIANDAA KUSHINDA AU KUSHINDWA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. N i  Ukweli usiopingika kuwa maisha  tuliyonayo yamejaa ushindani,hivyo ushindani hauepukiki tunakutana ...


Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Ni  Ukweli usiopingika kuwa maisha  tuliyonayo yamejaa ushindani,hivyo ushindani hauepukiki tunakutana nao kwenye kila kona ya maisha iwe ni uchumi,kazi,siasa,mahusiano.
Katika mashindano kuna matokeo ya aina mbili pekee kushinda na kushindwa hakuna droo kwenye maisha.
Kwa mantiki hiyo kama maisha ni ushindani tunapaswa kujiandaa si tu kujiandaa kushindana bali kujiandaa kushindana na kushinda.
Maisha yanafanana na mashindano ya kupiga mbio kwa lugha ya kigeni wanaita Marathon ambapo wapiga mbio ni wengi lakini washindi ni wachache.
Maandalizi ni muhimu kama tunahitaji kushinda kwenye kila jambo elimu,biashara .Mara nyingi mashindano hayana miujiza kushinda na kushindwa kunategemea na jinsi ulivyojiandaa.
Wahenga waliwahi kusema kuwa maisha fainali uzeeni .Unapofika umri Fulani unaanza kufaidi matunda ya juhudi zako ,kama hukuweka juhudi  inakua tofauti,kupata ushindi kunatokana na nguvu ya maandalizi.
“Usipojiandaa kushinda jiandae kushindwa” Anaeleza Msanii Fareed Kubanda katika wimbo wake wa siri ya mchezo akieleza umuhimu wa maandalizi.
Maisha yanahitaji mpangilio,mipango thabiti,mikakati na utekelezaji ambao ndio maandalizi ya kushinda katika maisha.
Watu wengi wanajiandaa kushindana lakini sio kushinda wanajikuta wamekua washiriki wa mashindano lakini sio washindi,Muhimu ni kujiandaa kushindana na kushinda.
Unapojiandaa kushindana na kushinda unatengeneza stamina ,ustahimilivu na uvumilivu wa kutosha ndani yako.
Haijalishi magumu unayoyapitia ,maumivu unayoyapata ,macho yako yatakua yanatazama kuelekea ushindi ulipo kuliko kutazama magumu na maumivu  hivyo utajikuta ukikaza mwendo kuyaelekea mafaniko ama ushindi.
Ukijiandaa kushindana na kushinda unatengeneza shabaha ndani yako kwani mara zote unauona ushindi ndani yako na nje.
Maandalizi yanatengeneza  picha ya ushindi katika moyo wako ,akili yako na si picha ya mashindano.
Unapoenda kushindana kichwani kwako una picha ya mashindano na si ya ushindi unaweza kuishia kuwa mshiriki wa mashindano na si mshindi.
Kujiandaa kushindana na kushinda kunatengeneza kiu ya kufikia ushindi ,tama,shauku ya kushinda  hilo linatengeneza msukumo wa ndani wa kuufikia ushindi ,msukumo ambao unazaa msukumo wa nje ambao ni bidii,juhudi,ubunifu na nidhamu.

Wanaoshindana kwenye kupiga Mbio ni wengi lakini anayechukua tuzo ni mmoja.
JIANDAE KUSHINDANA NA KUSHINDA.NAKUTAKIA USHINDI KATIKA MWAKA 2015

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top