Dkt
Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji akiongea kwenye kongamano la
uwekezaji kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika lililofanyika mjini
sumbawanga mwishoni mwa wiki. hawapo pichani washiriki wa kongamano hilo
Washiriki
wa kongamano la uwekezaji ambao ni wawekezaji kutoka ndani na nje ya
nchi wakifuatilia kwa umakini mjadala wa kongamano hilo kwenye uwanja wa
Nelsoni Mandela Mjini Sumbanga Mkoani Rukwa.
Na Kibada Kibada Rukwa.
Waziri
wa Uwekezaji na uwezeshaji Dkt Mary Nagu amezishauri Taasisi za Kifedha
hasa mabenki kupunguza riba inayotonzwa wakati wa kuomba mikopo ili
kuwezesha wawekezaji Mwekezaji wa ndani na nje kukopa na kupata mitaji
itakayomsaidia kuweza kuwekeza.
Alitoa
ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa Kongamano la Uwekezaji kwa
Mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika unaojumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi
na Kigoma lililofanyika kwenye viwanja vya Nelsoni Mandela Mjini
Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Kongamano
hilo lilihudhuriwa Viongozi mbalimbali, Mabalozi wanaowakilisha nchi
zao hapa nchiniWawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na
wananchi wa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika hasa wakazi wa mjini
Sumbawanga Mkoani Rukwa na lilifunguliwa na Makamu wa Rais Dkt Ghalib
Bilal.
Dkt
Nagu ambaye alikuwa mwenyekiti katika kongamano hilo amezishauri Taasisi
hizo za Kifedha kuangalia uwezekano wa kupunguza riba kama kweli
wanataka kumsaidia mtanzania wa kawaida kuondokana na umasikini.
Alaongeza
kuwa kama kweli wanataka kukuza uwekezaji na kumsaidia mtanzani ili
naye aweza kuwa na mtaji wa kuwekeza na kukuza uchumi ni vyema Taasisis
hizo zikaona namna ya kuweza kupunguza riba ili waweze kukopa na kuwa na
mitaji itakayosaidia kuwekeza,na iwapo wataendelea na taratibu zao za
kutoza riba kubwa watakuwa hawana nia wala lengo la kumkomboa mtanzani.
“Nawaombeni
muuangalie utaratibu huo wa namna ya kuweze kuwasaidia hawa wananchi
wanataka kujikomboa kuondoka na umasikini kwa kuomba mikopo kutoka
kwenye Taasisi zenu za kifedha”alieleza Waziri Nagu.
Awali
akiwasilisha mada katika warsha hiyo mwakilishi wa kutoka Benki ya NMB
iliyohusu taratibu za taasisi za kifedha katika suala la uwekezaji
kwenye ukanda wa ziwa Tanganyika Afisa masoko wa Banki ya NMB Richard
Makungwa kwa niaba ya Meneja wa Benki ya NMB alieleza kuwa ukanda wa
ziwa Tanganyika una fursa nyingi za uwekezaji kwenye mikoa hiyo ya Rukwa
,Katavi na Kigoma kutokana na Jiografia ya ukanda huo.
Makungwa
akaeleza kuwa Mkoa wa Rukwa kwa mjibu wa Sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2012 una watu wapatao 1,004,539 na eneo la kilometa za ukubwa
22,792 ambao unapakana na nchi ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo DRC ambapo shughuli za kiuchumi katika mkoa huo ni kilimo cha
mahindi mpunga,ulinaji asali kilimo cha ufuta,alizeti,uvuvi wa samaki,na
shughuli za uchimbaji madini.
Akizungumzia
Mkoa wa Katavi ambao kijiografia una ukubwa wa kilometa za mraba47,843
na idadi ya watu wapatao kwa mjibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka
2012 ina idadi ya watu wapatao 564,604 na unapakana na nchi ya Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo DRC na shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo,cha
mahindi,mpunga,ulinaji asali kilimo cha ufuta ,alizeti,pamoja na
shughuli za kitalii kutokana na kuwepo kwa mbuga ya wanayama pori ya
Katavi.
Na kwa
upande wa Mkoa wa Kigoma ambao jiografia yake inaonesha kuwa ina ukubwa
wa kilometa za mraba 37,040 inapakana na nchi ya jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo DRC,na Burundi ambao uchumi wake unategemea kilimo
cha kahawa,michikichi,mahindi,uvuvi,kilimo cha tumbaku,na utalii
kupitia hifadhi ya taifa ya Gombe na Mahale.
Wakazi
wa mikoa hiyo wanayonafasi kubwa ya kukuza uchumi wao kwa kuwa
wanazofursa kubwa za kiuchumi na wanashauri kukopa kwenye Taasisi za
kibenki ili kuweza kuwekeza katika fursa zilizopo kwenye ukanda huu wa
ziwa Tanganyika.
Makungwa
ameleza kuwa uchumi wa mikoa hii ya Rukwa, Kigoma na Katavi umekuwa na
ukipanda kila mwaka ambap mfano pato la mtu mmoja mmoja kwa miaka ya 90
hadi 2000 pato la kila mtu ni kubwa ukilinganisha na mkoa wa Kigoma.
Mikoa ya Rukwa na Katavi pato lake liko juu.
Akizungumzia
suala kuwekeza benki ya NMB amesema kuwa imeweza ni moja ya benki kubwa
kwa sasa kwa kuwa imeweza kutoa mikopo hadi shilingi bilioni 400 hadi
kufikia trioni 3.5 kwa sasa kwenye matawi zaidi ya 150 nchi nzima bado
inaendelea kufungua mataw hadi maeneo ya vijijini.na wana tarajia
kufungua matawi katika wilaya za Kalambo Mkoani Rukwa, Mlele Mkoani
Katavi na Kakonko Mkoani Kigoma.
Akaeleza
kuwa kwa mwaka 2013 kiasi cha shilingi bilioni 200 zimetolewa kwa mwaka
huu kwa ajili ya mikopo kwa wawekezaji na wajasiliamali waliokopo
kwenye benki hiyo.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Benki ya Tanzania alieleza kuwa ukanda huu una
rasilimali za aina mbalimbali kwenye ukanda huu,rasilimali hizo ni
ardhi nzuri yenye rutuba kwa shughuli za kilimo, gesi,mafuta,misitu na
madini ambapo tasisi za kifadha zinatakiwa zijikite katika ukanda huu
ili kuwekeza katika ukanda huu.
Hata
hivyo pamoja na kuwepo kwa fursa hiyo zipo changamoto za umasikini kwa
wananchi wa ukandda huu ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji, changamoto
ya kutowatumia wataalamu wa uchumi waliopo kwenye maeneo hayo hasa
kuwasaidia wananchi namna ya kutengeneza maandiko ya kuombea mikopo
kwenye mabenk nayo ni moja ya changamoto inayowakabiri wananchi wa
ukanda wa ziwa Tanganyika.
Serikali
kutosaidia kuanzisha benki za maendeleo ya kilimo kwenye ukanda huu ili
waweze kujikopesha mikopo itakayowasiadia kuendesha shughuli zao za
kukuza uchumi hasa kwenye kilimo.
Changamoto
nyingine ni mtazamo finyu wa mawazo ambapo inatakiwa mabadiliko hasa
kwa kubadili mtazamo wa kizazi kilichopo kwa kuweka mfumo mzuri wa
kifedha katika kukopo.
Vijiji
na kata kuwatambua vijana waliomaliza vyuo vikuu kuweza kuwakuwapa
elimu wananchi namna ya kuanzisha miradi ya ujasiliamali ili waweze
kukopesheka kwenye taasisi za kibenki
Akifunga
Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Salehe
Machibya ameleza kuwa Taasisi za kibenki zilizopo hapa nchi zinatoza
riba kubwa tofauti na nchi nyingine za Kiafrika hivyo ipo hasa kubwa ya
kuangalia upya Taasisi hizo kama wanataka kumsaidia Mtanzania.
Post a Comment