PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUPUNGUZA RIBA ILI KUWAINUA WANANCHI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Dkt Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji akiongea kwenye kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyik...

 

Dkt Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji akiongea kwenye kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika lililofanyika mjini sumbawanga mwishoni mwa wiki. hawapo pichani washiriki wa kongamano hilo
Washiriki wa kongamano la uwekezaji ambao ni wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wakifuatilia kwa umakini mjadala wa kongamano hilo kwenye uwanja wa Nelsoni Mandela Mjini Sumbanga Mkoani Rukwa.

Na Kibada Kibada Rukwa.

Waziri wa Uwekezaji na uwezeshaji Dkt Mary Nagu amezishauri Taasisi za Kifedha hasa mabenki kupunguza riba inayotonzwa wakati wa kuomba mikopo ili kuwezesha wawekezaji Mwekezaji wa ndani na nje kukopa na kupata mitaji itakayomsaidia kuweza kuwekeza.

Alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa Kongamano la Uwekezaji kwa Mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika unaojumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma lililofanyika kwenye viwanja vya Nelsoni Mandela Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Kongamano hilo lilihudhuriwa Viongozi mbalimbali, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchiniWawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na wananchi wa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika hasa wakazi wa mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa na lilifunguliwa na Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal.

Dkt Nagu ambaye alikuwa mwenyekiti katika kongamano hilo amezishauri Taasisi hizo za Kifedha kuangalia uwezekano wa kupunguza riba kama kweli wanataka kumsaidia mtanzania wa kawaida kuondokana na umasikini.

Alaongeza kuwa kama kweli wanataka kukuza uwekezaji na kumsaidia mtanzani ili naye aweza kuwa na mtaji wa kuwekeza na kukuza uchumi ni vyema Taasisis hizo zikaona namna ya kuweza kupunguza riba ili waweze kukopa na kuwa na mitaji itakayosaidia kuwekeza,na iwapo wataendelea na taratibu zao za kutoza riba kubwa watakuwa hawana nia wala lengo la kumkomboa mtanzani.

“Nawaombeni muuangalie utaratibu huo wa namna ya kuweze kuwasaidia hawa wananchi wanataka kujikomboa kuondoka na umasikini kwa kuomba mikopo kutoka kwenye Taasisi zenu za kifedha”alieleza Waziri Nagu.

Awali akiwasilisha mada katika warsha hiyo mwakilishi wa kutoka Benki ya NMB iliyohusu taratibu za taasisi za kifedha katika suala la uwekezaji kwenye ukanda wa ziwa Tanganyika Afisa masoko wa Banki ya NMB Richard Makungwa kwa niaba ya Meneja wa Benki ya NMB alieleza kuwa ukanda wa ziwa Tanganyika una fursa nyingi za uwekezaji kwenye mikoa hiyo ya Rukwa ,Katavi na Kigoma kutokana na Jiografia ya ukanda huo.

Makungwa akaeleza kuwa Mkoa wa Rukwa kwa mjibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 una watu wapatao 1,004,539 na eneo la kilometa za ukubwa 22,792 ambao unapakana na nchi ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC ambapo shughuli za kiuchumi katika mkoa huo ni kilimo cha mahindi mpunga,ulinaji asali kilimo cha ufuta,alizeti,uvuvi wa samaki,na shughuli za uchimbaji madini.

Akizungumzia Mkoa wa Katavi ambao kijiografia una ukubwa wa kilometa za mraba47,843 na idadi ya watu wapatao kwa mjibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ina idadi ya watu wapatao 564,604 na unapakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC na shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo,cha mahindi,mpunga,ulinaji asali kilimo cha ufuta ,alizeti,pamoja na shughuli za kitalii kutokana na kuwepo kwa mbuga ya wanayama pori ya Katavi.

Na kwa upande wa Mkoa wa Kigoma ambao jiografia yake inaonesha kuwa ina ukubwa wa kilometa za mraba 37,040 inapakana na nchi ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC,na Burundi ambao uchumi wake unategemea kilimo cha kahawa,michikichi,mahindi,uvuvi,kilimo cha tumbaku,na utalii kupitia hifadhi ya taifa ya Gombe na Mahale.

Wakazi wa mikoa hiyo wanayonafasi kubwa ya kukuza uchumi wao kwa kuwa wanazofursa kubwa za kiuchumi na wanashauri kukopa kwenye Taasisi za kibenki ili kuweza kuwekeza katika fursa zilizopo kwenye ukanda huu wa ziwa Tanganyika.

Makungwa ameleza kuwa uchumi wa mikoa hii ya Rukwa, Kigoma na Katavi umekuwa na ukipanda kila mwaka ambap mfano pato la mtu mmoja mmoja kwa miaka ya 90 hadi 2000 pato la kila mtu ni kubwa ukilinganisha na mkoa wa Kigoma. Mikoa ya Rukwa na Katavi pato lake liko juu.

Akizungumzia suala kuwekeza benki ya NMB amesema kuwa imeweza ni moja ya benki kubwa kwa sasa kwa kuwa imeweza kutoa mikopo hadi shilingi bilioni 400 hadi kufikia trioni 3.5 kwa sasa kwenye matawi zaidi ya 150 nchi nzima bado inaendelea kufungua mataw hadi maeneo ya vijijini.na wana tarajia kufungua matawi katika wilaya za Kalambo Mkoani Rukwa, Mlele Mkoani Katavi na Kakonko Mkoani Kigoma.

Akaeleza kuwa kwa mwaka 2013 kiasi cha shilingi bilioni 200 zimetolewa kwa mwaka huu kwa ajili ya mikopo kwa wawekezaji na wajasiliamali waliokopo kwenye benki hiyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Benki ya Tanzania alieleza kuwa ukanda huu una rasilimali za aina mbalimbali kwenye ukanda huu,rasilimali hizo ni ardhi nzuri yenye rutuba kwa shughuli za kilimo, gesi,mafuta,misitu na madini ambapo tasisi za kifadha zinatakiwa zijikite katika ukanda huu ili kuwekeza katika ukanda huu.

Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa fursa hiyo zipo changamoto za umasikini kwa wananchi wa ukandda huu ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji, changamoto ya kutowatumia wataalamu wa uchumi waliopo kwenye maeneo hayo hasa kuwasaidia wananchi namna ya kutengeneza maandiko ya kuombea mikopo kwenye mabenk nayo ni moja ya changamoto inayowakabiri wananchi wa ukanda wa ziwa Tanganyika.

Serikali kutosaidia kuanzisha benki za maendeleo ya kilimo kwenye ukanda huu ili waweze kujikopesha mikopo itakayowasiadia kuendesha shughuli zao za kukuza uchumi hasa kwenye kilimo.

Changamoto nyingine ni mtazamo finyu wa mawazo ambapo inatakiwa mabadiliko hasa kwa kubadili mtazamo wa kizazi kilichopo kwa kuweka mfumo mzuri wa kifedha katika kukopo.

Vijiji na kata kuwatambua vijana waliomaliza vyuo vikuu kuweza kuwakuwapa elimu wananchi namna ya kuanzisha miradi ya ujasiliamali ili waweze kukopesheka kwenye taasisi za kibenki

Akifunga Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Salehe Machibya ameleza kuwa Taasisi za kibenki zilizopo hapa nchi zinatoza riba kubwa tofauti na nchi nyingine za Kiafrika hivyo ipo hasa kubwa ya kuangalia upya Taasisi hizo kama wanataka kumsaidia Mtanzania.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top