Mgeni
rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwasili
ukumbini wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh.
Bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari na (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko
Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.Mwakilishi
wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akisaini
mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya Benki hiyo kwa ajili ya kuwakopesha
wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri
wa Fedha, Adam Malima. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki
ya CRDB, Martin Mmari na Wa pili kulia ni, Mwakilishi wa Umoja wa
Ulaya, Eric Beaume.
Mwakilishi
wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia)
akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei baada ya benki hiyo kusaini mkopo wa billion 43 na benki ya CRDB
kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Malima.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kushoto), Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin
Semunyu (wa pili kulia) wakiwa katika hafla ya uwekaji saini wa mkataba
wa mkpo wa sh. bilioni 43 na Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwakilishi
wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume (kulia) akibadilishana mawazo
na Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos
Milianitis (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB pamoja na wadau wengine.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa
hafla ya uwekaji saini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 kutoka Benki
ya Uwekezaji Ulaya.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
Meza Kuu.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akifuatilia kwa
makini hafla ya uwekaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 na
Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
Na Mwandishi Wetu
BENKI
ya CRDB imesaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 baina ya benki ya
uwekezaji Ulaya (E.I.B) kwa ajili ya kuwakopesha na kuwasaidia
wafanyabiashara wanaofanya shughuli za kukuza uchumi.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,
Dk. Charles Kimei alisema benki yake kwa kushirikiana na EIB imeamuwa
kusaidia jamii nchini hivyo mkataba huo ni mwanzo wa ushirikiano
endelevu utakaohamasisha upatikanaji wa ajira.
Alisema
kufanyakazi na benki ya EIB kutasaidia kukuza biashara katika maeneo
muhimu kama uvuvi, usindikaji wa chakula, usafiri, biashara pamoja na
huduma zote za kiuchumi.
“Mimi
kama kiongozi wa CRDB Tanzania ninamamlaka ya kusaidia hizi sehemu za
soko na kuongeza jitihada za kumaliza umaskini, pia kuongeza shughuli za
kiuchumi za wateja wetu ili kufikia lengo la kuongeza mapato katika
benki yetu,” alisema Kimei.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alisema mkataba huo pia
una lengo la kuisaidia benki ya CRDB katika kuendesha shughuli zake
mbalimbali.
Alisema
ni jambo la faraja kuona benki kama EIB imekubali kuiamini CRDB na
kuipa mkopo wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia
wafanyabiashara.
“Tunachokiamini
kuwa hii benki kutoka Ulaya siyo benki ndogo ni kati ya benki kubwa
zilizopo hapa duniani, sasa kama wamekuja hapa kwetu na wakaonyesha nia
njema ya kutusaidia endapo watabaini kuwa pesa zao azitatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa watavunjika moyo,” alisema.
Post a Comment