Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akitazama soko la Meru Curio
Craft maarufu kama masai market lilivyoteketea kwa moto ulianza majira
ya jana jioni ,kushoto ni Kamanda wa Jeshi la polisi Liberatus
Sabas.Picha na Ferdinand Shayo
Baadhi
ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni
lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa
kuamkia leo.
Wakazi wa Jiji la Arusha wakiangalia namna moto ulivoathiri soko hilo.
Bango la Soko hilo.
Hali si swari kabisa sokoni hapo.
Wengine wakiangalia kama watabahatika kuokoa chochote.
Wengine wakiokota mabaki ya mabati yaliyoungua.
Sehemu
ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina
la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la
kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo
na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika
kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za
kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo
ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka
hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto
na kusababisha hasara kwa wananchi.
"Sitakubali
kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa
uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama
Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo
cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku
yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto
kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
|
Post a Comment