Mkali wa Bongo fleva, Nasibu Abdul au maarufu kwa jina la Diamond akipozi.
ANAITWA
Nasibu Abdul au maarufu kwa jina la Diamond. Alizaliwa saa kumi na moja
jioni ya Oktoba 2, 1989 katika Hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya
Ilala jijini Dar es Salaam. Wazazi wake walimpa jina la Nasibu wakiamini
ni la bahati.
Diamond
aliongea hivi karibuni na safu hii ya Mjue Huyu ambapo aliweka wazi
mambo mengi ya maisha yake. Diamond akiwa hajapata ufahamu, yaani bado
mdogo, wazazi wake walitengana kwa sababu ambazo bado hazijawa wazi na
baba yake kumuacha na mama.
Kufuatia
hali hiyo, ilibidi mama yake ahamie kwa mama yake mzazi (bibi wa
Diamond), Tandale Magharibi, Dar. Hapo ndipo yakawa makazi ya mama huyo
na mwanaye.
Mnamo
mwaka 1995, Diamond alianza elimu ya awali katika Shule ya Chakula Bora
iliyopo Tandale- Uzuri. Mwaka 1996 alianza elimu ya msingi katika Shule
ya Msingi Tandale- Magharibi iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwaka
2000, Diamond akiwa darasa la tano alianza kupenda muziki, hivyo akawa
anakopi baadhi ya nyimbo za wasanii waliokuwa wakihiti ndani na nje ya
Bongo na kuimba yeye katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa kuliona hilo, mama yake alianza kumnunulia kanda za albamu za
wasanii tofauti hata kumwandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili
mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi.
Diamond alizidi kuupenda muziki ikabidi mama yake awe anampeleka kwenye matamasha mbalimbali ili mwanae apate nafasi ya kuimba.
Baadhi
ya ndugu walimjia juu mama huyo wakidai anamharibu mtoto badala ya
kumuhimiza masomo anamwingiza kwenye muziki ambao walidhani haukuwa na
faida yoyote katika maisha yake
hapana shaka kwa sasa waliokuwa wanandhani anapoteza muda kuimba katika matamasha sasa wanaamini kuwa muziki ni kazi inayoweza kumpa mtu heshima mbele ya jamii na pia kutoa ajira kwa wengine wengi
Post a Comment