PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NYOTA YA IVO MAPUNDA YAWAKA , AITWA TENA KENYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kipa wa Simba,Ivo Mapunda,PICHA|MAKTABA   Dar es Salaam. Klabu ya Gor Mahia ya Kenya inafikiria kumrudisha kipa wake wa zamani, Ivo Map...




Kipa wa Simba,Ivo Mapunda,PICHA|MAKTABA
 
Dar es Salaam. Klabu ya Gor Mahia ya Kenya inafikiria kumrudisha kipa wake wa zamani, Ivo Mapunda msimu ujao, wakati kiungo Jonas Mkude akisaini mkataba wa miaka mitatu kwa gharama Sh60 milioni kuitumikia Simba.

Kusaini kwa Mkude ni habari njema kwa wanasimba baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kiungo huyo anatakiwa Yanga na Azam. Wakati Mkude akimalizana na Simba upande wa Ivo inaonekana ni tofauti kwani uvumi umekuwa ukiendelea kuwa uongozi wa Simba una mpango wa kumrejesha Juma Kaseja aliyeko Yanga.

Kwa sababu hizo, uongozi wa Simba unaweza kuamua kuachana na Ivo kwenye dirisha dogo la usajili linalofunguliwa mwishoni mwa wiki.

Kumekuwa na taarifa kuwa Mapunda anaweza kutemwa Simba kwa madai ya kushuka kiwango chake baada ya kufungwa mabao mawili na Coastal Union kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu ambayo viongozi wa klabu hiyo wamekuwa wakidai kuwa yalikuwa mabao mepesi.

Mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier alisema jana kuwa walikuwa na wakati mzuri walipokuwa na kipa huyo, lakini akasajiliwa na Simba wakati mkataba wake ulipomalizika.

“Kwa kweli Ivo aliondoka vizuri na hata hivyo alitusaidia kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita.

“Alifanya kazi kwa kujitolea na hicho ndicho kinachotuvutia kumtaka endapo atamalizana na Simba. Kwa kweli hicho ndicho kilichomfanya awe miongoni mwa makipa bora Afrika Mashariki. Uwezo alionao si wa kukaa benchi kule Tanzania wala hapa (Kenya) au hata Uganda. Naamini bado tunahitaji huduma zake na hivyo tunaangalia uwezekano wa kumchukua muda wowote iwapo ataachana na Simba,” alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake, Mapunda alisema bado ana mkataba na Simba na anaheshimu mkataba huo na iwapo Gor Mahia watamhitaji, lazima wawasiliane na uongozi wa Simba.
“Nina furaha kuona kwamba ninaheshimika ndani na nje ya nchi kutokana na kazi ninayofanya. Namaliza mkataba wangu Mei mwakani baada ya mchezo wa mwisho wa ligi, kwa sasa niko chini ya Simba, hivyo Gor Mahia au klabu nyingine ikinihitaji inatakiwa kufuata utaratibu kwa kuiona Simba.”

Aliongeza: “Sina tatizo kuondoka Simba kwani mpira ndivyo ulivyo, kama wao wanaona hawahitaji tena kunitumia wafuate utaratibu waniache na si kuchafuliana jina.”
Hata hivyo, alisema Simba bado haijamwambia kama anaachwa na kusisitiza kuwa timu hiyo ingefanya busara kumwambia ukweli kwani anahitajika pia kwenye timu zingine.
“Nimecheza soka kwa miaka 15 na maisha yangu yamekuwa kwenye mpira, hivyo leo hii mimi kuondoka Simba siyo tatizo, kitu cha msingi ni taratibu zifuatwe na kama kuna madai tumalizane niondoke,” alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top