HABARI PICHA-NAIBU WAZIRI WA KILIMO GODIFREY ZAMBI AKIWEKA GUNIA KWENYE MASHINE YA KUSAFISHA MBEGU jijini arusha
Kampuni ya mbegu ya Seedco imezindua kiwanda kipya cha kuzalisha mbegu bora za mahindi na nafaka nyingine kitakachowasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na kupata mazao mengi.
Uzinduzi huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi ambaye alifungua rasmi kiwanda hicho ,Amesema kuwa tasnia ya mbegu ni tasnia muhimu katika ukuaji wa sekta ya kilimo hiyo amewataka wazalishaji mbegu kuongeza tija ili kukuza kilimo.
Ameeleza kuwa kampuni hiyo imetimiza matakwa ya serikali kwa kwa kuandaa na kuzalisha mbegu nchini badala ya kuagiza kutoka nje na kuzilipia kwa fedha za kigeni .
"Mbegu hizi zinazoandaliwa na kuzalishwa ndani ya nchi zinasambazwa kwa bei rahisi na wakulima wanazipata kwa bei rahisi tofauti na zile zinazoagizwa kutoka nje bei yake huwa juu" Alisema Waziri huyo
Mwakilishi wa Bodi ya Seedco,Profesa Kalunde Simbuge amesema kuwa mbegu hizo bora zinazozalishwa na kiwanda hicho zitawasaidia wakulima kuzalisha chakula cha kutosha na ziada kwa ajili ya kuuza na kujipatia kipato.
Profesa Kalunde anafafanua kuwa wakulima wana jukumu kubwa la kuilisha jamii hivyo wanahitaji mbegu bora zinazoendana na mazingira yao.
Mkulima kutoka Wilaya ya Hai Joel Nkya amesema kuwa ufunguzi wa kiwanda hicho utakidhi mahitaji ya mbegu bora hasa kwa wakulima walioko vijijini.Amewashauri wakulima wenzake kuacha kuona kuwa mbegu halisi ni ghali na kuingia kwenye mtego wa kuuziwa mbegu feki kwa bei rahisi.
Post a Comment