Home
»
»Unlabelled
» WAGONJWA WA KISUKARI KUPATWA UPOFU WA MACHO
Wagonjwa wa kisukari mkoani Kilimanjaro wameshauriwa
kwenda kumwona mtaalamu wa magonjwa ya macho mapema kutokana na kile
kilichoelezwa wapo hatarini kupatwa na matatizo ya macho.
Daktari wa macho na mratibu wa macho mkoani humo Dr Hilda Shangali
ametoa wito huo baada ya kugundua jamii nyingi hapa nchini ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro
hawana uelewa kuwa matatizo ya sukari mwilini huweza kusababisha matatizo ya
upofu kwa uharaka zaidi.
Aidha Dr Shangali alibainisha matatizo hayo kuwa ni pamoja
na mtoto wa jicho na uvujaji wa damu mishipa ya nyuma,hivyo kuhamua kutoa wito
huo kwa jamii hususani wagonjwa wa kisukari kuwahi matibabu ya macho kabla ya
kupatwa na upofu wa macho.
“Uvujaji wa damu mishipa ya nyuma ni hatari sana kwani hauna
dalili zinazoonekana wala mgonjwa hapatwi na maumivu yoyote yale hivyo
niwahimize tu wawahi wataalamu wa macho ili kuziba ufa kuliko kujenga ukuta”Alisema
Dr Shangali.
Sanjari na hayo Hilda shangali alitoa pia wito kwa waratibu
wa macho Taifa kufanya hamasa kwa wagonjwa wa kisukari kufika mapema kwa
wataalamu wa macho kupata tiba na ushauri
“ Ili kwa pamoja tufanikiwe kufikisha elimu kwa jamii ya Tanzania
kuwa wagonjwa wa kisukari wapo hatarini kupatwa na upofu ama matatizo mengine
ya macho niwatake waratibu wa macho Taifa
nao waendeleze na kufanya hamasa kwa jamii kihusu hili”Alimalizia Shangali.
Ili pia kudhibitisha hayo gazeti la MBIU YA JAMII ilizuru
baadhi ya vituo vya kutoa huduma ya afya mkoani hapo na kugundua licha ya wagonjwa
hao kutokua na uelewa yakuwa wapo hatarini kupatwa na upofu pia wengi wao
wameshindwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu aina ya vyakula
wanavyopaswa kula kutokana na kile walichokieleza kukabiliwa na changamoto za
kiuchumi pamoja na ndugu na jamaa wanaowahudumia nao pia hawaelewi umuhimu wa
wagonjwa wao kutumia vyakula hivyo kila mara.
About Author

Advertisement

Recent Posts
- The Maasai Families in Longido District allegedly use baptism ceremonies to conceal FGM practices17 Sep 20240
By our Reporter in Longido Some Maasai families in Longido District, Arusha Region ar...Read more »
- Tanzanian Shillings 6.56 Trillion Investment in the JNHPP Project Bears Fruits for the Nation14 Sep 20240
By Our ReporterThe Public Investments Committee (PIC) of Parliament visited the construction site of...Read more »
- 35 teams set to battle in Chem Chem Cup 2024: Sh78 million up for grabs10 Sep 20240
By Mussa Juma, MaipacBabati. A total of 35 teams will participate in the 2024 Chem Chem Cup, costin...Read more »
- Mwiba holdings Donates house for Health Workers and 194 bicycles to Meatu students.29 Aug 20240
By Our Staff Writer in MeatuMwiba Holdings Ltd, a tourism and conservation investment company ...Read more »
- Mount Kilimanjaro porters' jobs in jeopardy due to foreign influence and controversial practices29 Aug 20240
KPAP's influence has shifted the tourism market, with foreign agents favoring their affiliates over ...Read more »
- Tanzania ramps up health education amid Mpox threat25 Aug 20240
By Staff WriterIn a bold move to safeguard Tanzania from the looming threat of Mpox, the Ministry o...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.