Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi
funguo za Basi dogo kwa Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani,
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga(kushoto). Basi hilo
litatumiwa na Wanafunzi katika ziara mbambali za Mafunzo hivyo kuondoa
kero kubwa ya Usafiri shuleni hapo.
Kaimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Emmanuel Lwinga akijaribisha kuwasha gari jipya
lililokabidhiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir
Minja(hayupo pichani) katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne
Bwawani Sekondari yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2014.
Muonekano
wa Basi dogo lenye Na. MT. 0341 lililokabidhiwa leo Oktoba 22, 2014 na
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika
Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari katika ziara
mbalimbali za Mafunzo.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(aliyevaa skafu) akiwa
meza Kuu amesimama na Viongozi mbalimbali Waalikwa wakati Wahitimu
Wakiimba Wimbo Maalum wa Shule katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato
cha Nne Bwawani Sekondari leo Oktoba 22, 2014(wa pili kushoto) ni
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(wa
kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula (wa kwanza kulia) ni Kaimu Mkuu
wa Shule ya Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel
Lwinga.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa
Mhitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kidato cha Nne Bwawani
Sekondari leo Oktoba 22, 2014. Jumla ya Wahitimu 95 wametunukiwa cheti
cha kuhitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule hiyo inayomilikiwa na
Jeshi Magereza, Mkoani Pwani.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi
katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari
yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2014 Mkoani Pwani.
Sehemu
ya Wahitimu katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne, Bwawani
Sekondari wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa
Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kikundi
cha Wasanii kinachoundwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari kikijiandaa
kutumbuiza mbele ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya
Kidato cha Nne Shule ya Bwawani Sekondari, Mahafali hayo yamefanyika leo
Oktoba 22, 2014, Mkoani Pwani.
Mama
mzazi wa Mhitimu wa Kidato cha Nne kutoka familia ya Kifugaji ya
Kimasai akimbusu mkono Mtoto wake ambaye amehitimu Elimu ya Kidato cha
Nne katika Shule inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, Bwawani Sekondari
iliyopo Mkoani Pwani. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa na
Wahitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha
Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza.
Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014 katika Bwalo la Bwawani
Sekondari, Mkoani Pwani
Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Post a Comment