Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Hoteli
ya Diaoyutai iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili hotelini hapo. Mama
Salma ameambatana na mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye amewasili
nchini China tarehe 21.10.2014 kwa ziara ya kiserikali.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya
mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi
tarehe 21.10.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa
viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation (CNOOC),
wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa
Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea
makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe
22.10.2014. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi
baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil
Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji
wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu
ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China
wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la CNOOC la China
katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati
walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe
22.10.2014.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na
Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji
cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi
kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe
22.10.2014.
Vifijo baada ya ufunguzi wa Kijiji
cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi
kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe
22.10.2014.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika
zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi
wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum
mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa
Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li
na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana
Joseph Kahama.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum
mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa
Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li
na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana
Joseph Kahama.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake kwenye kijiji cha
sanaa za Afrika mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika kumbukumbu
yake.
Waanzilishi
wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han
Rong wakimkabidhi zawadi ya mchoro wa Tingatinga Rais Dkt. Jakaya
Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe
22.10.2014. Picha na John Lukuwi
Post a Comment