PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI ZA IRINGA: MATAPELI WATUMIA SARE ZA POLISI KUJITAFUTIA KIPATO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  JESHI la Polisi mkoani Iringa, linawashikilia matapeli wawili waliokuwa wanatapeli wananchi katika mkoa huo na mkoa wa Morogoro kuhusu ...
 


JESHI la Polisi mkoani Iringa, linawashikilia matapeli wawili waliokuwa wanatapeli wananchi katika mkoa huo na mkoa wa Morogoro kuhusu namna ya kujiunga na Jeshi hilo kuwapatia fedha ili waweze kufanikisha zoezi hilo kwa kipindi cha muda mrefu kinyume cha sheria.

Aidha, mmoja wa watuhumiwa hao amegundulika kuwa ni Mwalimu aliyekuwa anajifanya Askari wa Jeshi hilo akiwa na sare, huku kiwa na bosi wake mmiliki wa studio moja (jina limehifadhiwa) katika eneo la Kihesa mkoani Iringa.

Kamnda wa Polisi mkoani humo, Ramadhani Mungi, ameiambia FikraPevu leo Juni 3, 2014 kuwa Jeshi lake lilipata taarifa kutoka kwa wananchi juu ya utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaojitambulisha kuwa wanatoka katika Jeshi hilo na kuamua kuweka mtego na kuwanasa watu hao.

“Kuna mmoja ana yunifomu za Jeshi la Polisi, huyi alikuwa anaenda kwa wananchi na kuwaeleza kuwa kama kuna mtu anataka kumwingiza kijana wake katika mafunzo ya Jeshi la Polisi yeye anauwezo wa kumuunganishia, kitu ambacho ni kinyume na sheria”



Aidha, alisema katika uchunguzi wa awali wamegundua kuwa nguo za Jeshi hilo zilizokuwa zinatumiwa na matapeli hao “ziliibiwa" kwa Polisi mmoja ambaye hawawezi kumtaja kwa sasa na alisharipoti siku za nyuma mkoani humo na wanaendelea kufuatilia kuona kama tukio la kupotea kwa nguo hizo na tukio hilo zinahusiana vipi.

“Tutawafikisha Mahakamani kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kwa kujifanya Askari Polisi, kwa kukutwa na sare za Jeshi, na kufikishwa Mahakamani kwa wizi was are za Jeshi, kwa hiyo vitu vyote hivyo vinaweza kuwafanya wawe na kesi nyingi za kujibu” alikaririwa na FikraPevu.

Amesema kufuatilia tetesi hizo waliweka mtego ulifanikiwa katika eneo la Ipogolo, ambapo askari huyo ‘feki’ alikuwa amepiga kambi ya utapeli kwa kuwadanganya wazazi wenye shida ya kuwafanikishia watoto wao kujiunga na Jeshi hilo.

“Vijana hao wawili akiwemo Goodluck Mbehele (21) ambaye mkazi Ikula Mtua Wilaya ya Kilolo alipata kusoma kozi ya ualimu mkoani Shinyanga na alikuwa akijifanya Askari na muda wote amekuwa akivaa sare za Jeshi la Polisi”



Mungi, amesema kijana huyo akiwa na mwenzake amewatapeli watu wengi katika mikoa ya Iringa na Morogoro na kuwa mtu wa mwisho kutapeliwa alitoa kiasi cha Tsh 900,000 na kutumia njia ya kujidai kuwa mtu mmoja ambaye yupo katika eneo la tukio anampigia bosi wake ambaye naye ni Askari feki aliyemtaja kwa jina moja la Mbehale.

Kumbumbu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2013, siku chache baada ya Trafiki ‘feki’ mwenye ‘Cheo cha Sajenti’ kukamatwa jijini Dar es Salaam akiongoza magari, mapya yalizidi kuibuka baada ya Jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwakamata watu (7) waliotuhumiwa kuwa majambazi wakiwa wamevalia sare za Jeshi hilo wakiwa na vyeo tofauti.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top