PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha AJTC Kimeeneshaa semina ya ujasiriamali Itakayofanyika kwa siku tatu chuoni hapo
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Akifungua semina ya ujasiriamali mapema leo. pic...

Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Akifungua semina ya ujasiriamali mapema leo. picha na KEPHAS ILANI










Mkurugenzi wa chuo chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha bwana Joseph Mayagila amefungua semina ya siku tatu ya ujasiriamali leo itakayomalizika siku ya ijumaa chuoni hapo.
Bwana Joseph Mayagila amesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana kwa wanafunzi wote kwa sababu dunia ya sasa imejengeka katika misingi ya ujasiriamali.

Alisema kuwa ili mtu yeyote afanikiwe kibiashara ni lazima ajue kupanda mbegu, thamani ya muda pamoja na mavuno ambayo ni matokeo ya kupanda mbegu.

“Unaweza kuhangaika sana kwa lengo  la kupata fedha mbegu, kwa kuwa mbegu hizo zitazalisha fedha nyingi zaidi kupitia mbegu hiyo”
Semina hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa kozi zote chuoni hapo ikiwemo kozi ya uandishi wa  habari, ualimu,sekretari pamoja na kozi ya kompyuta.

Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na wakufunzi wa chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya mikakati ya kibiashara,  na mada ya huduma kwa wateja iliwasilishwa na bw, Christian Ndege na mada ya Miongozo ya mjasiriamali, iliwasilishwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo bw, Andrea Ngobole.  

Bwana Mayagila alisema kuna kuuuza na kununua lakini sio kila mtu anaweza kuuza na kuwataka wote kujenga fikra zao katika kuuza ila waweze kujenga maisha yao

Alisema kama mtu anataka kufanikiwa maishani na kutaka kununua vitu vya thamani ni lazima mtu ajipange vizuri katika  kuuza
“Duniani kuna kuuza na kununua huwezi kukwepa kununua lakini  sio kila mtu anaweza kuuza, unaweza kuuza mawazo, jambo na bidhaa” Alisema Mayagila
Mayagila aliwashauri wanafunzi wake kujiunga   kwenye taasisi za kifedha kwani mkopo ni fedha mbegu na zitawasaidia  kufanikisha biashara zao na kuzaa zaidi

Amehitimisha ufunguzi wa  semina hiyo kwa kusema kwamba ili mtu yeyote afanikiwe ni lazima kusoma vitabu mbalimbali 
“Nyumba isiyyo na vitabu ni mfu, akili isiyopenda kusoma ni mfu pia ,ili uweze kufanikiwa nilazima ulipe gharama za kufanikiwa”

Na baada ya uzinduzi huo semina ilianza rasmi  ambapo Bw. Onesmo Mbise alifundisha maada ya Bussiness Planing na kuzungumuzia zaidi mikakati mahususi kuhusu biashara

   Bw. Onesmo Elia Mbise akito a maada mapema leo.Picha na Benson Mremi

 Mkufunzi wa pili Bw. Christian Ndege yeye alifundisha somo la Customer Care na kueleza mbinu mbalimbali za kuvutia wateja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri , kumheshimu na kumtambua kuwa ni bosi na kumwomba radhi pale tu unapomkosea

Nae kwa upande wake Bw. Andrea Ngobole aliwasilisha somo la tatu kwa siku ya leo kuhusu misingi/miongozo ya mjasiriamali Bw. Ngobole amesema mjasiriamali yeyote ni vyema kuwa na marafiki  wajasiriamali ili kufanikiwa kupata taarifa mbalimbali kuhusu Biashara

             Bw. Andrea Ngobole Akiwasilisha maada juu ya muongozo wa misingi ya mjasiriamali . Picha na Benson Mremi

Wakati huo huo pia ametaja mambo ambayo mjasiriamali anapaswa kuyaepuka  ikiwa ni pamoja na kulaumu, starehe, kuamini uchawi, umbea na mengine mengi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kufika mbali na kufanikiwa kibiashara


Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha AJTC wakiwa makini kufufuatlia moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina ya Ujasiriamali mapema jana

Aidha wanafunzi walio wengi chuoni hapo wameipoke kwa furaha semina hiyo ambayo
            itaendelea tena mapema kesho asubuhi saa 3 kamili
credit: this is habari blog

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top